Chama tawala nchini Msumbiji kilitangazwa kuwa kimeshinda uchaguzi wenye utata wa urais na wabunge kwa kishindo siku ya Alhamisi huku wafuasi wa upinzani wakifanya maandamano katika miji kadhaa ambayo yalisababisha takriban kifo cha mtu mmoja.
Daniel Chapo kutoka chama cha Frelimo, ambacho kimekuwa madarakani kwa nusu karne, alipata karibu asilimia 71 ya kura za urais Oktoba 9, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (CNE) ilitangaza.
Kiongozi wa upinzani Venancio Mondlane, ambaye alijitangaza mshindi na kudai kuna makosa mengi alipata juu kidogo ya asilimia 20 ilisema.
Forum