Makamu Rais wa Botswana Ndaba Gaolatha, atahudumu pia kama Waziri wa fedha, Rais mpya Duma Boko alisema leo Jumatatu akitangaza nafasi za kwanza za mawaziri katika baraza lake.
Kuotokana na matokeo ya kushangaza kufuatia uchaguzi wa mwanzoni mwa mwezi huu, ushirika wa Rais Boko wa Umbrella for Democratic Change ulikiondoa madarakani chama ambacho kilitawala taifa hilo la kusini mwa Afrika kwa takriban miongo sita.
Wachambuzi wanasema ongezeko la malalamiko ya kiuchumi hasa miongoni mwa vijana, yalichangia ushindi mkubwa wa Boko. Katika kipaumbele cha juu cha Gaolatha itakuwa kuinua ukuaji wa uchumi, ambapo miradi ya shirika la kimataifa la fedha-IMF itapungua kwa asilimia moja mwaka huu, hasa kutokana na kupungua kwa uzalishaji wa almasi.
Forum