Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Novemba 21, 2024 Local time: 13:05

Wanawake watatu wachaguliwa kuwa wabunge wa taifa Botswana


Mafisa wa uchaguzi wakipanga makaratasi ya kuwa kwa akiji ya uthibitisho huko Gaborone Oktober 31, 2024. Picha na Monirul Bhuiyan / AFP
Mafisa wa uchaguzi wakipanga makaratasi ya kuwa kwa akiji ya uthibitisho huko Gaborone Oktober 31, 2024. Picha na Monirul Bhuiyan / AFP

Ni wanawake watatu pekee waliochaguliwa katika Bunge la Taifa la Botswana katika uchaguzi mkuu wa wiki iliyopita, ambao ulishuhudia mabadiliko ya madaraka kwa chama tofauti cha siasa kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 58.

Wanawake watatu waliochaguliwa ni miongoni mwa wagombea 28 wanawake wanaowania viti vya ubunge.

Helen Manyeneng wa chama kipya kinachotawala, Umbrella for Democratic Change (UDC), ni mmoja wa wabunge wanawake watatu katika Bunge la 61.

Chama cha UDC kilipata ushindi dhidi ya Chama cha Botswana Democratic Party ambacho kimekuwa madarakani tangu nchi hiyo ilipopata uhuru mwaka 1966.

Wafuasi wa chama cha Botswana Congress Party (BCP) huko Gaborone Septemba 28, 2024.
Wafuasi wa chama cha Botswana Congress Party (BCP) huko Gaborone Septemba 28, 2024.

Manyeneng anasema wanawake wanakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo umaskini katika juhudi zao za kushinda nyadhifa za kisiasa.

“Sisi wanawake tunazidiwa na umaskini. Tuna hadhi ya chini katika jamii na kiuchumi nchini Botswana, kama wanawake. Serikali iliyopita haikuonyesha nia ya kisiasa ya kutusaidia”

“Nadhani kama mbunge mpya mwanamke niliyechaguliwa, nitatetea uwezeshaji wa wanawake kiuchumi” aliongeza.

Uchaguzi mkuu uliopita wa Botswana mwaka 2019, pia ulishuhudia wanawake watatu pekee waliochaguliwa kuingia bungeni.

Manyeneng anasema mfumo dume katika jamii, ambapo wanaume wana udhibiti mkubwa wa fedha na maamuzi, unazuia ushiriki wa wanawake

“Wanawake wana shauku sana. Wanawake wanaweza na suala lililopo ni nani anayepaswa kuwainua, nani anapaswa kuwasaidia” amesema Manyeneng

“Kama ukiruhusu hali ya kuwa chini ya mwanamme, namaanisha mtu anayekusaidia kifedha, hatokuruhusu kusimama katika nafasi ya kisiasa. Wanaume wengi wanataka kudhibiti. Hawataki kudhibitiwa au hawataki kushirikiana udhibiti huo na sisi” aliongeza.

Kiongozi wa upinzani wa Botswana Duma Boko akipeana mkono na mwanamke baada ya chama chake kushinda
Kiongozi wa upinzani wa Botswana Duma Boko akipeana mkono na mwanamke baada ya chama chake kushinda

Shirika la kikanda lisilo la kiserikali la Gender Links lilitoa ripoti kuhusu Botswana kabla ya uchaguzi wa Oktoba 30, ambao uliibua wasiwasi unaoelezea kukosa sauti za wanawake katika siasa.

Mshauri wa masuala ya jinsia, Pamela Dube anasema Botswana imefanya hatua ndogo sana kuwawezesha wanawake.

Dube amesma, “Ni hali ya kusikitisha. Imekuwa hivi kwa muda mrefu sana, miaka 58 baadaye tuna wanawake watatu pekee bungeni. Tumezungumza sana juu ya suala hili, kutokana na jamii ya mfumo dume ambayo tunayo Botswana, haiamini wanawake wanaweza kuongoza hasa katika maeneo kama siasa.”

Aidha anasema mfumo wa uchaguzi wa Botswana unatoa kikwazo kwa wanawake wanaotaka kuwania nafasi za uongozi.

Pia amesema “Gender Links imefanya kazi kubwa katika hilo, hiyo inaonyesha kuwa nchi ambazo hazijaendelea bado zinashikilia kwa mara ya kwanza mfumo wa uchaguzi wa baada ya uchaguzi, una wanawake wachache katika ofisi za kisiasa wakati nchi ambazo zimepitisha uwakilishi wa uwiano zinasimamia kupata wanawake zaidi katika ofisi za kisiasa”.

Siku ya Jumatano, rais mpya aliyechaguliwa Duma Boko alitumia kipindi maalum kuwataja wanawake wengine watatu katika bunge la taifa.

“Tulitaka kuwafikia kwa upana iwezekanavyo ili kuwaleta wanawake vijana hasa wenye ujuzi na kujulikana katika jamii. Na kisha bila shaka, tulipaswa kuangalia ili kuongeza idadi ya wanawake bungeni.” Amesema.

Uteuzi huo maalum unamaanisha kuwa bunge la Botswana lina uwakilishi wa wanawake kwa asilimia 8.9, bado liko chini ya asilimia 30 katika lengo la Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika-SADC.

Forum

XS
SM
MD
LG