Balozi wa Marekani nchini Tanzania amesisitiza hataacha kuzungumzia maswala ya demokrasia na haki za binadamu kinyume na alivyoagiza rais Samia Suluhu Hassan.
Afrika itawakilishwa na mabondia 24 katika Michezo ya Olimpiki ya 2024 iliyopangwa kufanyika Paris, Ufaransa, kuanzia Julai 27 hadi Agosti 10.
Takriban tikiti milioni tisa tayari zimeuzwa - milioni sita kati yao kwa chini ya Euro 50.
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi wa mawaziri wawili akiwemo Januari Makamba (waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki) katika mabadiliko madogo ya baraza la mawaziri, ofisi yake ilisema.
Katika hotuba iliyosubiriwa kwa hamu kubwa na Wamarekani , hatimaye JD Vance alisimama mbele ya jukwaa kujitambulisha na kuelezea ajenda za chama cha Republican katika mkutano wa chama cha Republican unaokamilika hii leo Milwauke, Wisconsin.
Msukumo wa kuunda Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka kufuatia shinikizo la vijana nchini Kenya hatimaye umezaa matunda baada ya Rais William Ruto kusaini Mswada wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka wa 2024 kuwa sheria.
Rais wa Marekani Joe Biden na Rais wa zamani wa Marekani na mgombea urais kwa tiketi ya chama cha Republikan Donald Trump wakishiriki katika mdahalo wa CNN wa wagombea urais wa uchaguzi wa mwaka 2024 katika studio za Kituo cha Televisheni cha CNN huko Atlanta, Georgia, Juni 27, 2024.
Waziri Mkuu wa Haiti Garry Conille aliahidi kwamba, hatua kwa hatua, udhibiti wa nchi ungerejeshwa huku maafisa wa polisi wa kwanza wa Kenya waliotumwa kukabiliana na ghasia za magenge watakapowasili nchini mwake.
Mwaka 2024 dunia inaadhimisha miaka 25 tangu kupitishwa kwa azimio la kuzuia Aina Mbaya Sana ya Ajira kwa Watoto.
Marais wa nchi tano za Afrika na wakuu wa serikali wamehudhuria mkutano wa Kilele wa kujadili ubora wa udongo na mbolea barani Afrika, wakitoa wito wa uwepo wa mkakati wa pamoja, hatua za pamoja na uwekezaji ili kuiwezesha Afrika kuzalisha chakula cha kutosha.
Mahakama ya kijeshi katika mji wa Goma huko Kivu Kaskazini Mashariki mwa Congo imewahukumu kifo maafisa nane wa jeshi la Congo, FARDC kwa tuhuma za kukimbia vita na kutoheshimu sheria za kijeshi.
Mwaka huu Sherehe za Siku ya Kimataifa ya Wafanyakazi zina hisia ya dharura ya kujitolea upya kwa haki za kijamii, wakati tunapopitia kipindi kigumu, ikiwa ni pamoja na mabadiliko ya hali ya hewa na mabadiliko ya haraka katika sehemu za kazi kutokana na maendeleo ya teknolojia.
Mafuriko makubwa yameyakumba maeneo mengi ya Afrika Mashariki ambayo yanakabiliwa na mvua za mfululizo, Burundi ikiomba msaada wa kimataifa wa kuisaidia kupambana na maafa hayo.
Wakulima nchini Kenya waliopewa mbolea ghushi watafidiwa na serikali ya Kenya baada ya kampuni moja kutajwa kuwahadaa wakulima na hivyo kuiweka serikali katika hali ngumu kufuatia Sakata hilo.
Gavana wa Jimbo la Maryland, Wes Moore, ameweka wazi kuwa hapakuwa na kitendo chochote cha kigaidi baada ya daraja kuu katika mji wa Baltimore kubomoka Jumanne asubuhi wakati meli iliyobeba mizigo kugonga nguzo yake.
Wawakilishi wa Burundi katika michuano ya mwaka huu ya Ligi ya Mpira wa Kikapu Afrika- BAL katika mashindano yanayofadhiliwa na Chama cha mpira wa Kikapu NBA tawi la Afrika Jumatatu walipoteza ushiriki wao baada ya kukataa kuvaa jezi yenye nembo ya Visit Rwanda.
Mungano wa asasi za kiraia nchini Senegal umetangaza kuundwa kwa mungano mpya na vyama vya kisiasa ili kutayarisha uchaguzi wa rais kabla ya tarehe 2 mwezi Aprili.
Rais wa zamani wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi, amefariki leo Alhamisi akiwa na umri wa miaka 98, vyanzo vya habari nchini Tanzania vimeeleza.
Mwili wa raia wa Tanzania umepatikana ukielea katika Mto Miami Marekani Jumanne asubuhi na idara husika zikithibitisha kuwa mwili huo ni wa mtu aliyeanguka kutoka katika mashua mwishoni mwa juma.
Wahifadhi wa mazingira na wanyama pori wa Afrika Kusini wameonya Jumanne kwamba kuna ongezeko kubwa la ujangili wa wanyama pori, wakiwemo wanyama takriban 500 wameuawa mwaka jana.
Pandisha zaidi