Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 29, 2024 Local time: 14:50

Waziri Mkuu wa Haiti aahidi kurejesha udhibiti wa nchi hiyo


Waziri Mkuu wa Haiti Garry Conille akiongea katika mkutano wa waandishi wa habari katika makazi yake rasmi huko Port-au-Prince, Haiti, Juni 25, 2024.
Waziri Mkuu wa Haiti Garry Conille akiongea katika mkutano wa waandishi wa habari katika makazi yake rasmi huko Port-au-Prince, Haiti, Juni 25, 2024.

Waziri Mkuu wa Haiti Garry Conille aliahidi kwamba, hatua kwa hatua, udhibiti wa nchi ungerejeshwa huku maafisa wa polisi wa kwanza wa Kenya waliotumwa kukabiliana na ghasia za magenge watakapowasili nchini mwake.

Mshauri wa Usalama wa Taifa wa Kenya Monica Juma alisema kikosi hicho kitaweka kipaumbele katika kuwalinda raia, kuruhusu watu kutembea, na kuwepo njia za usafiri wa bidhaa na misaada ya kibinadamu, na kulinda taasisi za serikali.

Kikosi hiki cha kulinda amani kilichokuwa kikisubiriwa kwa muda mrefu, kinachoongozwa na Kenya kiliwasili katika nchi ya Caribbean mnamo Jumanne (Juni 25).

Vita vya magenge nchini Haiti sasa vimewakosesha makazi watu nusu milioni.

Takriban watu milioni tano wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula.

Makundi yenye silaha, ambayo sasa yanadhibiti sehemu kubwa ya mji mkuu, yameunda muungano mpana huku yakitekeleza mauaji yaliyoenea, utekaji nyara na unyanyasaji wa kingono.

Habari hii inatokana na vyanzo mbalimbali vya habari

Forum

XS
SM
MD
LG