Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 21:57

Polisi wa Kenya waondoka kwenda Haiti


Kikosi cha Kenya kitakachoongoza ujumbe wa kimataifa kukabiliana na ghasia za magenge ya Haiti kimeondoka Nairobi, Jumatatu usiku, waziri wa mambo ya ndani Kithure Kindiki amesema.

“Ni heshima kuona kundi la kwanza la Polisi ambao ni sehemu ya ujumbe wa kihistoria wa Umoja wa Mataifa kwa Haiti, likiondoka” Kindiki amesema katika taarifa yake.

Kenya ilijitolea kupeleka takriban polisi 1,000 ili kuleta utulivu Haiti pamoja na wafanyakazi kutoka nchi kadhaa, lakini hatua hiyo imekumbwa na changamoto za kisheria katika taifa hilo la Afrika Mashariki.

Baadhi ya polisi 400 wameondoka Nairobi, saa 4 na dakika 50 usiku kwa kutumia ndege ya shirika la Kenya, afisa katika wizara ya mambo ya ndani ameiambia AFP.

Forum

XS
SM
MD
LG