Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 22:00

Kikosi cha polisi cha Kenya kupelekwa Haiti Jumanne


Picha ya maktaba ya polisi wa Kenya.
Picha ya maktaba ya polisi wa Kenya.

Kikosi cha polisi wa Kenya kitaondoka kuelekea Haiti Juni 25, ili kuongoza Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kukabiliana na magenge, licha ya malalamishi yaliyowasilishwa mahakamani dhidi ya hatua hiyo, vyanzo vya serikali na polisi vimesema Jumapili.

Kenya ilisema kuwa ingetuma polisi 1,000 ili kurejesha udhabiti nchini Haiti kwa ushirikiano na wenzao kutoka mataifa mengine, lakini hatua hiyo imekumbwa na vizingiti vya kisheria. Rais wa Kenya William Ruto amekuwa kwenye mstari wa mbele kuunga mkono mpango huo, wakati akiahidi mapema mwezi huu kwamba ungeanza ndani ya wiki kadhaa.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Oktoba mwaka jana liliidhinisha kupelekwa kwa kikosi hicho, lakini mahakama moja ya Kenya ikachelewesha hatua hiyo Janurari. Kando na Kenya, mataifa mengine yaliyoelezea nia yao ya kujiunga na kikosi hicho ni pamoja na Benin, Bahamas, Bangladesh, Barbados na Chad.

Marekani inatoa ufadhili, pamoja na msaada wa kiufundi, bila kutuma wanajeshi wake moja kwa moja kwenye taifa hilo masikini zaidi la Caribbean. Shirika la kimtaifa la haki za binadamu la Human Rights Watch limeelezea wasi wasi wake kuhusu hatua hiyo wakati pia likihoji ufadhili wake.

Forum

XS
SM
MD
LG