Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 22:43

Makamanda wa polisi wa Haiti watembelea Kenya


Picha ya polisi wa Kenya ambao wamepangwa kupelekwa Haiti mwishoni mwa Juni
Picha ya polisi wa Kenya ambao wamepangwa kupelekwa Haiti mwishoni mwa Juni

Timu ya makamanda wa polisi kutoka Haiti, Jumanne wamekutana na mkuu wa polisi wa Kenya, jijini Nairobi, kabla ya upelekaji wa polisi wa Kenya kwenye taifa hilo la Caribbean lililokumbwa na ghasia, hatua inayotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi Juni

Kenya inaongoza ujumbe wa walinda amani kutoka mataifa tofauti, chini ya ufadhili wa Umoja wa Mataifa, ili kukabiliana na magenge yaliyopo nchini humo yaliyosababisha vifo vya maelfu ya watu na kupelekea wengine zaidi ya 360,000 kukimbia makwao.

“Tunategemea msaada wenu,” Afisa wa polisi amemueleza mkuu wa polisi wa Kenya Inspekta Japhet Koome mjini Nairobi , wakati polisi walipokuwa wakikabiliana na waandamanaji wanaopinga mswaada unaolenga kuongeza ushuru. Kwa upande wake, Koome amesema kuwa, “Tuko tayari kuja na kusaidia kwa namna yoyote ile.”

Maafisa hao wa Haiti pia wamekutana na makamanda wa kikosi cha Kenya cha polisi 1,000 kitakachopelekwa nchini humo kwa ajili ya kulinda amani. Kenya pia itatoa mafunzo kwa polisi wa Haiti, na idara ya polisi imesema kuwa wajumbe wa Haiti waliopo Kenya, baada ya kukutana na mkuu wa Polisi walipelekwa kwenye kambi ambako mafunzo hayo yatatolewa.

Forum

XS
SM
MD
LG