Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 18:29

Waziri mkuu wa Haiti atoka hospitalini


Waziri mkuu mpya wa Haiti, Garry Conille, Jumapili ameruhusiwa kutoka hospitalini akiwa katika hali nzuri baada ya kulazwa kwa tatizo la kupumua hapo jana vyanzo viwili vya serikali viliiambia shirika la habari la AFP.

Conille, Jumapili alasiri alitoa video akiueleza umma kwamba ametoa video hiyo ili kuwahakikishia watu kwamba anaendela vizuri.

Chanzo cha serikali, kilichozungumza bila kutambulishwa kimeiambia AFP kwamba waziri mkuu alikuwa akisumbuliwa na pumu. Conille, 58, aliteuliwa kuwa waziri mkuu na baraza la mpito la Rais wa Haiti, Mei 29 na kuapishwa Jumatatu iliyopita.

Wajiubu muhimu unaomkabili ni kurejesha hali sawa ya kisiasa, usalama na huduma za kibinadamu ambazo zimekuwa mbaya katika taifa hilo masikini katika ukanda wa magharibi wa dunia, na kuweka mazingira ya kufanyika uchaguzi wa kwanza toka mwaka 2016.

Forum

XS
SM
MD
LG