Baraza la mpito la Haiti limeteua baraza jipya la mawaziri Jumanne, kuashiria hatua ya mwisho ya kujenga upya serikali itakayoongoza nchi iliyogubikwa na magenge yenye silaha.
Msemaji wa serikali Kettia Marcellus, amethibitisha kuwepo kwa baraza jipya la mawaziri na mawaziri wake kwa shirika la habari la The Associated Press.
Carlos Hercules, wakili wa Waziri Mkuu Garry Conille, ameteuliwa kuwa waziri wa sheria na usalama wa umma.
Conille mwenyewe atakuwa waziri wa mambo ya ndani, huku Jean Marc Berthier Antoine ateuliwa kuwa waziri wa ulinzi.
Haiti inapambana na magenge yanayo dhibiti takriban asilimia 80 ya mji mkuu wa Port-au-Prince.
Inajiandaa kwa kupokea kikosi cha polisi kutoka Kenya kinachoungwa mkono na Umoja wa Mataifa kinachotarajiwa kwasili wiki kadhaa zijazo.
Forum