Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 23:02

Polisi wa Kenya kupelekwa Haiti ndani ya wiki zijazo


Polisi wa Kenya wakipiga doria katika mitaa ya Nairobi, Machi 12, 2024. Picha ya AP
Polisi wa Kenya wakipiga doria katika mitaa ya Nairobi, Machi 12, 2024. Picha ya AP

Polisi wa Kenya watapelekwa nchini Haiti kukabiliana na magenge ya uhalifu pengine ndani ya wiki zijazo, rais wa Kenya William Ruto alisema Jumapili, licha ya pingamizi za mahakama ambazo zilichelewesha mchakato huo.

Kenya imekubali kuongoza kikosi kinachoungwa mkono na Umoja wa Mataifa kulinda taifa hilo la Caribbean, linalokumbwa na machafuko, umaskini na ukosefu wa uthabiti wa kisiasa.

Taifa hilo la Afrika mashariki linapanga kupeleka maafisa 1,000 wa polisi kwa ajili ya operesheni hiyo pamoja na polisi wengine kutoka nchi nyingine kadhaa.

“Wananchi wa Haiti labda wanasubiri, kwa neema ya Mungu, labda kufikia wiki ijayo au wiki itakayofuata, tutatuma maafisa wetu wa polisi kurejesha amani,” Ruto alisema katika hotuba wakati wa ziara katikati mwa Kenya Jumapili.

Azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa mwezi Oktoba mwaka jana liliidhinisha kupelekwa kwa kikosi hicho lakini mahakama ya Kenya mwezi Januari ilichelewesha mchakato huo.

Mahakama ilisema serikali haikuwa na mamlaka ya kupeleka maafisa wa polisi nje ya nchi bila makubaliano ya awali.

Lakini chama kidogo cha upinzani nchini Kenya kiliwasilisha kesi mpya kujaribu kuzuia mchakato huo. Mahakama kuu ya Kenya inatazamiwa kusikiliza kesi hiyo tarehe 12 Juni.

Kando na Kenya, nchi nyingine ambazo zilielezea nia ya kujiunga na kikosi hicho ni pamoja na Benin, Bahamas, Bangladesh, Barbados na Chad.

Forum

XS
SM
MD
LG