Pia inatoa fursa kuwakumbusha wadau wote kuboresha utekelezaji wa mikataba miwili ya msingi ya ajira kwa watoto – Mkataba Na. 182 na Mkataba Na. 138 unaohusu umri wa chini kuajiriwa au kufanyishwa kazi (1973).
Licha ya kuwa hatua kubwa zimechukuliwa kwa miaka kadhaa sasa katika kupunguza ajira kwa mtoto, katika miaka ya hivi karibuni imeshuhudiwa mienendo ya kimataifa kurejesha nyuma mafanikio haya, ikisisitiza kunahitajika shinikizo kuunganisha juhudi hizi katika kuharakisha hatua za kutokomeza ajira kwa watoto katika hali zake zote..
Kufuatia kupitishwa kwa Malengo ya Maendeleo Endelevu 8.7, jumuiya ya kimataifa imeweka azma ya kutokomeza ufanyishwaji ajira kwa watoto katika hali zake zote ifikapo mwaka 2025.
Umoja wa Mataifa unaeleza kuwa sasa ni wakati muafaka kufanya hatua ya kutokomeza ufanyishwaji kazi watoto inafikiwa kiuhakika.
Tangu mwaka 2000, kwa takriban miongo miwili, dunia ilikuwa inapiga hatua imara katika kupunguza ajira kwa watoto.
Lakini katika miaka kadhaa iliyopita, migogoro, mizozo na janga la COVID – 19, limezitumbukiza familia nyingi zaidi katika umaskini – na kulazimisha mamilioni ya watoto kuingia katika ajira.
Ukuaji wa uchumi haujakuwa wenye kutosheleza, na wala haujajumuisha vya kutosha, kuziondolea shinikizo ambalo familia nyingi na jamii zinapitia na hivyo kuwafanya wageukie ajira kwa watoto.
Hivi leo, watoto milioni 160 bado wanafanyishwa kazi. Hiyo ni kwa kila watoto kumi mmoja anafanyishwa kazi duniani kote.
Bara la Afrika liko juu zaidi kati ya kanda mbalimbali yote mawili kwa asilimia ya watoto wanaofanyishwa kazi – moja ya tano – na idadi ya watoto kikamilifu wanaofanyishwa kazi – milioni 72.
Chanzo cha habari hii ni Umoja wa Mataifa.
Forum