Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 13:45

Tanzania yafuta sherehe za Siku ya Uhuru, yatumia fedha ya maadhimisho kusaidia watoto wenye mahitaji maalum


Rais Samia Suluhu Hassan
Rais Samia Suluhu Hassan

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amefuta sherehe za Siku ya Uhuru zilizokuwa zifanyike Ijumaa na kuelekeza kuwa bajeti iliyotengwa kwa ajili ya shughuli  hiyo badala yake itumike kujenga mabweni ya watoto wenye  mahitaji maalum.

Sherehe za Miaka 61 ya Uhuru zingegharimu dola laki 445, fedha ambazo zitatumika hivi sasa kujenga mabweni nane katika shule za msingi kote nchini.

Waziri wa Nchi, George Simbachawene, Jumatatu alisema fedha hizo tayari zilikuwa zimetolewa kwa ajili ya mradi huo..

Alisema badala ya kuwepo magwaride na maadhimisho mengine ya kitaifa, nchi hiyo ya Afrika Mashariki itafanya kumbukumbu ya Siku ya Uhuru kwa kuandaa makongamano ya umma kuhusu maendeleo.

“Midahalo na mikutano itatanguliwa na ratiba mbalimbali za viongozi wa mikoa na wilaya kufanya shughuli za kijamii katika maeneo tofauti ikiwemo kusafisha mahospitali, shule, makazi ya wazee na vikundi vya wale wenye mahitaji maalum,” alisema.

Kwa kawaida, sherehe za Siku ya Uhuru zinaadhimishwa kwa mwembwe na dhifa za kitaifa.

Hata hivyo hii si mara ya kwanza kwa Tanzania kufuta sherehe hizo.

Makamu Rais Samia Suluhu wa Tanzania na Rais John Magufuli wakizungumza kwa simu na Rais Kenyatta, Machi 17, 2021. (Photo by Ericky BONIPHACE / AFP)
Makamu Rais Samia Suluhu wa Tanzania na Rais John Magufuli wakizungumza kwa simu na Rais Kenyatta, Machi 17, 2021. (Photo by Ericky BONIPHACE / AFP)

Mwaka 2015, rais wa wakati huo John Magufuli alifuta sherehe mbalimbali na kupeleka fedha katika ujenzi wa barabara katika makao makuu ya kibiashara, Dar es Salaam.

Mwaka 2020, alifanya hivyo tena na kuelekeza kuwa bajeti kama hiyo itumike kununua vifaa vya afya.

Rais wa sasa, Samia, ni mwanamke wa kwanza kushikilia wadhifa wa urais nchini Tanzania.

Siku za nyuma alivuma kwa kuwaamuru maafisa wa polisi wenye vitambi kuvishughulikia ili waweze kuwa na ufanisi katika kazi zao.

Miongo kadhaa kabla ya kupata madaraka ya juu, alifanya kazi kama afisa maendeleo katika serikali ya Zanzibar.

Pia alikuwa ni meneja wa mradi wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani la UN na baadae kuwa mkurugenzi mtendaji wa taasisi kivuli inayosimamia asasi zisizo za serikali huko Zanzibar.

Pia siku za nyuma alihudumu katika nafasi ya waziri wa ajira kwa vijana, wanawake na watoto, na amezungumza hadharani akiwashawishi wanawake wa Tanzania na wasichana kuzifikia ndoto zao.

Chanzo cha habari hii ni Kituo cha televisheni cha al-Jazeera

XS
SM
MD
LG