Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Novemba 22, 2024 Local time: 01:43

Mfumo wa elimu Afrika Kusini washindwa kuwasaidia watoto masikini


Wanafunzi wa kike katika shule ya msingi ya Mbuyisa Makhubu iliyoko Soweto, Afrika Kusini. Picha na Picha na GULSHAN KHAN / AFP.
Wanafunzi wa kike katika shule ya msingi ya Mbuyisa Makhubu iliyoko Soweto, Afrika Kusini. Picha na Picha na GULSHAN KHAN / AFP.

Mfumo wa elimu nchini Afrika Kusini umeshindwa kuwasaidia watoto maskini sana kwa mujibu wa wazazi, waalimu na vijana wenyewe.

Watoto wengi wamelazimika kutumia saa nyingi kutembea kutoka na kwenda shule kila siku, mara nyingi katika mazingira hatari sana. Inadaiwa kuwa wamechoka sana, na hawawezi kutimiza uwezo wao wa kielimu.

Asubuhi katikati ya wiki katika kaya ya Nhlangothi katika kijiji kidogo huko Starford KwaZulu-Natal ni muda wa harakati nyingi kwa ndugu watano ambao wanajitayarisha kwenda shule.

Luyanda Hlali, anachukua kuni ambazo ziliwekwa usiku uliopita, anazichanganya na mavi ya ng’ombe na kuanza kuwacha moto kwa ajili ya kuchemsha maji katika kijumba kidogo cha matope.

Hawezi kulala kwa muda mrefu, anatakiwa kufanya kazi za nyumbani na kujitayarisha kwenda shule – ambayo iko katika mji wa uchimbaji makaa wa Dundee, kilometa 10 kutoka kijijini kwake.

Wakati wa majira ya baridi, anakumbana na giza, baridi kali na safari hatari kwa msichana mdogo ambaye anatembea kupitia kwenye msitu kabla ya kuweza kuipata barabara.

Watoto wa kike wa shule ya msingi ya Mbuyisa Makhubu, huko Soweto.
Watoto wa kike wa shule ya msingi ya Mbuyisa Makhubu, huko Soweto.

“Naamka na kuianza siku yangu nyakati za saa kumi na nusu alfajiri nakwenda kuchukua kuni na kuwasha moto, halafu naoga na kuvaa nguo na kuondoka kiasi cha kama baada ya saa 11 hivi.” Luyanda Hlali ambaye ni mwanafunzi wa darasa la tisa ambaye anatembea kwenda shule.

“Kwa kawaida nafika shule nyakati ya saa moja asubuhi na nikiwasili nakuwa nimechoka. Mara nyingi najitahdi kuwa makini katika kile ambacho mwalimu anakisema na mara nyingine najikuta nimesinzia. Waaalmu wanaponiita, ninachoweza kuwaeleza ni kwamba nimechoka.”aliongeza mwanafunzi huyo.

Hlali ni mmoja wa wanafunzi zaidi ya 200,000 katika jimbo la KwaZulu-Natal ambao wanashida ya usafiri wa kuwafikisha shuleni kwao.

Hlali na ndugu zake wanaishi katika sehemu duni yenye msongamano pamoja na bibi yao Bongiwe Nhlangothi.

Ana wasi wasi kwamba mjukuu wake hapewi fursa nzuri ya masomo kwasababu mahitaji ya watoto kama yeye kwa kawaida yanapuuzwa.

Bongiwe Nhlangothi alisema “Kwanza kabisa unahitaji kufikiria ni kwamba muda mwingi sana, sina chakula cha kuwapa wajukuu zaidi kama kifungua kinywa. Wanaondoka kwenda shule wakiwa na njaa na tumaini lao ni kwamba wanaweza kupata chochote ambacho kipo waweze kula wanapofika shule”

Na kuongeza kuwa “wanaondoka nyumbani mapema sana ili wawahi darasani, lakini wanakuwa wamechoka sana wakati wanapowasili shule. Unatarajia wahudhuria dara na kuwa makini sana kwa kile ambacho waalimu wanawafundisha huku watoto wakiwa wamechoka?”

Mfanyakazi wa ustawi wa jamii Bongeka Ndaba akiwa na watoto wa Shule ya Msingi ya Zamuthule, Kwazulu-Natal.
Mfanyakazi wa ustawi wa jamii Bongeka Ndaba akiwa na watoto wa Shule ya Msingi ya Zamuthule, Kwazulu-Natal.

Mtaalamu wa saikolojia Melinda du Toit anasema tatizo moja ni ukosefu wa usawa na maskini ambao hawawezi kumudu kuishi maeneo ya mjini kujitahidi kuboresha maisha yao.

Anasema watoto kimwili hawawezi kusoma vizuri wakati wakiwa wamechoka na wananyimwa elimu stahiki.

Melinda du Toit alisema, “Kwa watoto hawa, wanaanza mapema sana, kwahiyo hawapati kulala mpaka mwisho. Kwahiyo kinachotokea ni kuwa ubongo wao unakuwa umechoka, Na haijalishi una akili kiasi gani, ni mwerevu vipi, ubongo ni kama kompyuta, na unafanya kazi kwa njia ya kipekee.”

Katika jimbo hilo zaidi ya asilimia 30 ya watu hawan ajira na wanategemea misaada ya ustawi wa jamii.

Wanasema kama wakilipa ada ya usafiri kama randi 350 kwa mwezi basi hawawezi kununua chakula.

Watoto wakiwa wamevaa sare za shule huko Soweto
Watoto wakiwa wamevaa sare za shule huko Soweto

Naye afisa wa serikali ya mtaa, Mathew Ngcobo anasema baadhi ya njia za kwenda shule si nzuri hata kidogo.

“Watoto upande huu wa mto wanalazimika kwenda mbali zaidi upande mwingine wa mto. Kuliwahi kutokea tukio moja wakati gari ilichukuliwa na maji wakati wa mvua kubwa na iligundulika inaelea hapa na mto ulikuwa umefurika.” Alisema Ngcobo.

“Nimezungumza na wazazi wengi katika eneo hili na wanasema ni hatari sana kuwavusha watoto upande wa pili wa mto. Wamelazimika kuwaomba jamaa zao, marafiki ambao wanaishi upande mwingine wa mto kuwachukua watoto wao ili waweze kuwa na uwezo wa kufika shule kwa usalama.”alisema afisa huyo.

Takwimu za karibuni za serikali zinaonyesha kwamba shule 1148 huko KwaZulu-Natal peke yake zinasubiri orodha ya mabasi ya shule.

Idara ya Elimu ya KwaZulu-Natal imekataa kuhojiwa kwa ajili ya habari hii.

Forum

XS
SM
MD
LG