Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Septemba 28, 2024 Local time: 10:25

Afrika Kusini kuondoa wanadiplomasia wake Israel


Serekali ya Afrika Kusini, Jumatatu imesema itawaita nyumbani wanadiplomasia wake kutoka Israel, ikielezea wasiwasi wake kutokana na hali ya Gaza.

Pretoria pia imesema nafasi ya balozi wa Israel, nchini humo inazidi kua mbaya kwa siku hadi siku, ikimshutumu mwanadiplomasia huyo kutoa maoni makali kwa watu wanaoikosoa Israel.

Waziri katika ofisi ya rais, Khumbudzo Ntshavheni, aliuambia mkutano na wanahabari bila kutoa taarifa za kina kwamba, serekali ya Afrika Kusini imeamua kuondoa wanadiplomasia wote kutoka ubalozi wa Tel Aviv.

Pretoria, kwa kipindi kirefu imekuwa ikiunga mkono harakati za Palestina, ambapo chama tawala ANC kimekuwa kikihusisha na harakati zake za kipindi cha ubaguzi wa rangi.

Toka tukio la Oktoba 7, la Hamas, kushambulia Israel, kumekuwa na mivutano ya kidiplomasia kwa wanaounga mkono ama kukosoa upande mwengine wa mgogoro wa Israel na Hamas.

Forum

XS
SM
MD
LG