Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 12:22

Mawaziri 40 wa Afrika kufanya mazungumzo na Marekani huko Johannesburg


Kamishna wa AGOA, Albert Muchanga (Kulia) akikumbatiana na Waziri wa Biashara na Viwanda wa Afrika Kusini Ebrahim Patel (Kulia) AGOA huko Johannesburg Novemba 2, 2023. Picha na GUILLEM SARTORIO / AFP.
Kamishna wa AGOA, Albert Muchanga (Kulia) akikumbatiana na Waziri wa Biashara na Viwanda wa Afrika Kusini Ebrahim Patel (Kulia) AGOA huko Johannesburg Novemba 2, 2023. Picha na GUILLEM SARTORIO / AFP.

Mkutano wa kibiashara kati ya Afrika na Marekani umeanza nchini Afrika Kusini siku ya Alhamisi, huku Pretoria na Washington zikirekebisha uhusianowao baada ya mzozo kuhusu shutuma kwamba Afrika Kusini inajihusisha na Russia.

Mawaziri kutoka nchi zipatazo 40 za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara zinazonufaika na Sheria ya Ukuaji na Fursa kwa Afrika, au AGOA, watafanya mazungumzo ya siku tatu na wajumbe kutoka Marekani huko Johannesburg.

Uchaguzi wa Afrika Kusini kuwa mwenyeji wa mkutano huo unaofanyika kila mwaka umekuwa "ishara ya kujitolea kwetu kwenye uhusiano wetu wa pande mbili," naibu msaidizi wa waziri wa mambo ya nje wa Marekani anayehusika na masuala ya Afrika Joy Basu, aliliambia shirika la habari la AFP.

Iliidhinishwa na Bunge la Marekani mwaka 2000, AGOA ndiyo msingi wa sera ya uchumi na biashara ya Marekani katika bara la Afrika.

Mkataba huo unatoa nafasi kwa nchi ambazo zinakidhi vigezo vya kidemokrasia vinavyo tathminiwa kila mwaka.

Utamalizika mwaka 2025, wakati kukiwa na mpango mdogo wa kuwa na mrithi, mazungumzo yanatarajiwa kulenga uwezekano wa upanuzi.

Uhusiano kati ya Washington na Pretoria umekuwa si mzuri kutokana na vita vya Ukraine, huku kukiwa na shutuma kwamba Afrika Kusini, ambayo imesema inataka kutoegemea upande wowote, imekuwa karibu na Russia.

Rais wa Marekani Joe Biden akiwa na Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa katika Ikulu ya Marekani mjini Washington, DC, Septemba 16, 2022. Picha na SAUL LOEB / AFP.
Rais wa Marekani Joe Biden akiwa na Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa katika Ikulu ya Marekani mjini Washington, DC, Septemba 16, 2022. Picha na SAUL LOEB / AFP.

Biashara chini ya mkataba huo inachangia asilimia 21 ya mauzo ya nje ya Afrika Kusini kwa mwaka kwenda Marekani, ambayo ni kuanzia bidhaa za magari hadi malighafi na mwaka 2022 yalikuwa na thamani ya takriban dola bilioni tatu.

Katika taarifa yenye kali isiyo ya kawaida mwezi Mei, balozi wa Marekani nchini Afrika Kusini, Reuben Brigety, alidai kuwa meli ya mizigo ya Russia ilipakia silaha na risasi kwenye kituo cha jeshi la wanamaji cha Cape Town.

Jopo huru lililoteuliwa na Rais Cyril Ramaphosa kuchunguza suala hilo tangu wakati huo limehitimisha kwamba hakuna ushahidi wa kupendekeza silaha zilipakiwa kwenye meli hiyo.

Chanzo cha habari hii ni Shirika la habari la AFP

Forum

XS
SM
MD
LG