Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 01:22

Wahamiaji 1,300 kutoka Afrika wawasili Uhispania


Meli ya Uokoaji ya Bahari ya Uhispania "Salvamar Adhara" ikiikabilia mashua iliyowabeba wahamiaji katika kisiwa cha El Hierro huko Uhispania Oktoba 21, 2023. Picha na STRINGER / AFP.
Meli ya Uokoaji ya Bahari ya Uhispania "Salvamar Adhara" ikiikabilia mashua iliyowabeba wahamiaji katika kisiwa cha El Hierro huko Uhispania Oktoba 21, 2023. Picha na STRINGER / AFP.

Mamlaka inasema zaidi ya wahamiaji 1,300 kutoka Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara wamefika katika visiwa Canary huko Uhispania katika bahari ya Atlantiki, mwishoni mwa wiki hii.

Meli moja ilikuwa imebeba rekodi ya watu 321. Rekodi nyingine iliwekwa mapema mwezi huu wakati wahamiaji 8,561 walipowasili katika visiwa hivyo, wiki mbili za mwanzo za mwezi Oktoba.

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uhispania Fernando Grande-Marlaska ameihusisha rekodi ya idadi ya watu wanaowasili na kuyumba kisiasa kwa eneo la Sahel ambako kumekuwa na mapinduzi kadhaa.

Wahamiaji hao kwa ujumla hawataki kuishi katika visiwa hivyo, lakini badala yake waangazia kupata maisha bora kwa ajili yao na familia zao barani Ulaya au sehemu nyingine duniani.

Baadhi ya taarifa za habari hii zilitoka shirika la habari la Reuters na AFP.

Forum

XS
SM
MD
LG