Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 20:35

Marekani 'Kubadilisha' Mchakato wa Ugavi wa Madini Afrika unaotawaliwa na China


Rais wa China Xi Jinping (kulia) na Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa (kushoto) wakiwa katika mkutano na viongozi wa China na Afrika huko Johannesburg Agosti 24, 2023. Picha na ALET PRETORIUS / POOL / AFP.
Rais wa China Xi Jinping (kulia) na Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa (kushoto) wakiwa katika mkutano na viongozi wa China na Afrika huko Johannesburg Agosti 24, 2023. Picha na ALET PRETORIUS / POOL / AFP.

Afrika ni eneo jipya la mapambano kwa ushawishi huku Washington ikiimarisha juhudi za kuanzisha msururu wa ugavi madini ili kuepuka kuitegemea China.

Beijing inatawala mchakato wa madini muhimu kama vile cobalt, lithiamu na rasilimali nyingine kutoka katika bara hilo ambayo yanahitajika katika mabadiliko ya nishati safi na utengenezaji wa magari ya umeme.

Lakini katika mkutano wa wakuu wa nishati ya kijani Afrika wiki hii mjini Cape Town, ambao ulifanyika pembeni ya Wiki ya Mafuta Afrika, watu wachache walikuwa tayari kulizungumzia moja kwa moja.

Alipoulizwa kama Marekani ilikuwa ikijaribu kukaribiana na China, mmoja wa wazungumzaji katika jopo hilo, naibu waziri mdogo wa Mambo ya Nje ya Mareknai katika Ofisi ya Rasilimali za Nishati, Kimberly Harrington, alisema kwamba Washington ilikuwa inaangalia kuhusu "mabadiliko.”

Kwa upande wake, mjumbe mwenzake wa jopo Chiza Charles Newton Chiumya, mkurugenzi wa Umoja wa Afrika wa viwanda, madini, ujasiriamali na utalii aliiambia Sauti ya Amerika kuwa hataki kutumia neno "kushindana" kuelezea mitazamo ya nchi za Magharibi na China lakini alikubali kuna "maslahi mengi" katika madini muhimu barani Afrika.

Ubalozi wa China mjini Washington pia ulikuwa na mtizamo wake ulipoulizwa kama China inajiona iko katika ushindani na Marekani kwa ajili ya maliasili.

Wachambuzi huru, hata hivyo, walikuwa na mtizamo tofauti. China imefanya ni ‘kipaumbele cha juu kupata soko kwa madini muhimu takriban miongo miwili iliyopita na kuunga mkono mkakati huo kwa uwekezaji mkubwa wa diplomasia ya umma na miundombinu barani Afrika - ambayo mengi [yalikuja] kupitia deni la muda mrefu," alisema Tony Carroll, profesa katika programu ya masomo ya Kiafrika katika Chuo Kikuu cha Johns Hopkins, alipozungumza na VOA mapema mwaka huu.

Forum

XS
SM
MD
LG