Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 02:03

Rais wa China Xi akutana na maseneta wa Marekani, ajadili uhusiano na vipi utaathiri 'hatma ya binadamu'

Kiongozi wa Walio Wengi katika Baraza la Seneti la Marekani Chuck Schumer (kushoto) akisalimiana na Rais wa China Xi Jinping kabla ya kuanza kwa mkutano wao wa pamoja huko katika ukumbi wa Great Hall of the People mjini, Beijing on October 9, 2023.

Rais wa China Xi Jinping amesema Jumatatu uhusiano kati ya China na Marekani utaathiri “ Hatma ya binadamu” alipokutana na kundi la maseneta wa Marekani mjini Beijing.

Rais wa China Xi Jinping na Kiongozi wa walio wengi katika Baraza la Seneti Marekani wakihudhuria kikao cha pamoja katika Ukumbi wa Great Hall of the People huko Beijing, Jumatatu, Octoba 9, 2023. (Foto: Andy Wong/Pool via REUTERS)

Kiongozi wa walio wengi katika Baraza la Seneti Chuck Schumer ni afisa wa juu wa Marekani kwenda China wakati Washington inataka kupunguza mivutano na Beijing, akioongoza ujumbe wa watu sita.

Jinsi China na Marekani zinavyoshirikiana katika kukabiliana na ulimwengu wa mabadiliko na misukosuko ndivyo vitaamua mustakabali na hatima ya mwanadamu , Xi alisema hayo alipokutana na schumer katika ukumbi wa Beijing wa great Hall of the people.

Kwa upande wake Schumer alimwambia Xi “ nchi zetu kwa pamoja zitabadilisha muongo,” “ ndio maana tunatakiwa kudhibiti uhusiano wetu na kwa heshima, alisema.

Wakati huohuo waziri wa mambo ya nje wa Marekani Anthony Blinken, waziri wa fedha na wa biashara Janet Yellen na Gina Raimondo pamoja na mjumbe maalumu wa maswala ya mabadiliko ya hali ya hewa John Kerry wote walitembelea China mwaka huu.

Forum

XS
SM
MD
LG