Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 06:57

Taiwan yagundua uwepo wa ndege za kivita 39 za China na manowari


Wanajeshi wawili wakishusha bendera ya taifa la Taiwan.
Wanajeshi wawili wakishusha bendera ya taifa la Taiwan.

Taiwan Jumatatu imesema ilikuwa imegundua kuwepo kwa ndege za kivita 39 za China na manowari inayobeba ndege hizo karibu na kisiwa hicho baada ya manowari ya Marekani ya mashambulizi na meli ya Canada kusimama kwa muda  kwenye mlango  wa bahari wa Taiwan wakati wa wikiendi.

Kati ya Jumapili na Jumatatu asubuhi, ndege za kivita 26 na manowari 13 zilikuwa katika harakati kwenye kisiwa hicho, wakati ndege nyingine 13 zilionekana mapema saa za asubuhi ya siku ya Jumatatu, kulingana na wizara ya ulinzi ya Taiwan.

Manowari ya China ya Shandong ilionekana Jumatatu kiasi cha kilomita 111 kusini mashariki mwa eneo la Eluanbi lililoko kusini zaidi ya Taiwan, ikielekea mashariki zaidi na kuingia eneo la Western Pacific kwa ajili ya mafunzo, wizara hiyo iliongeza kusema.

China inaiangalia Taiwan kama jimbo lililojitenga na imeapa kukiweka kisiwa hicho chini ya utawala wake kwa njia yoyote muhimu, ikiwemo kukikamata kijeshi.

Katika miaka ya karibuni, Beijing imeelekeza shinikizo la kijeshi na kisiasa kwa Taiwan, mara kwa mara ikifanya mazoezi ya kijeshi au kupeleka ndege za kivita zikifanya fujo katika anga yao ikiwa sambamba na mazungumzo yoyote ya kidiplomasia yanayofanyika na Taipei

Taiwan ilisema ndege 22 kati ya 39 zilizoshuhudiwa hivi karibuni zilivuka mstari wa median katika upenyo wa bahari wa Taiwan, njia nyembamba ya majini iliyoko kati ya kisiwa hicho na China.

“Jeshi hilo linafuatilia kwa karibu hali hiyo na imeamuru ndege za kivita, manowari na mifumo ya makombora ya ardhini kukabiliana na tishio lolote,” wizara ya ulinzi ya Taiwan ilisema katika taarifa yake.

Siku ya Jumamosi, China ilisema vikosi vyake vilikuwa “katika uangalizi endelevu” baada ya manowari mbili za Marekani na Canada kupita katika upenyo wa bahari ya Taiwan.

Marekani ilisema meli hizo mbili zilikuwa Arleigh Burke-class guided-missile destroyer USS Ralph Johnson na HMCS Ottawa, kusimama kwa kwa manowari hizo kunaonyesha dhamira ya Marekani na washirika wetu na wadau wengine kuwepo Indo-Pacific iliyokuwa huru na wazi.

Marekani na washirika wake wa Magharibi wameongeza “uhuru wa kuwepo manowari hizo” zikivuka katika mlango wa bahari ya Taiwan na eneo lenye mivutano la bahari ya South China Sea kusisitiza kuwa maeneo hayo ya bahari ni ya kimataifa, ikiikasirisha Beijing.

Mwezi Aprili, Beijing ilifanya mazoezi ya kivita ikiwa ni majaribio ya kukizingira kisiwa hicho mwezi Aprili baada ya Tsai kukutana na Spika wa Baraza la Wawakilishi la Marekani Kevin McCarthy huko California.

Chanzo cha habari hii ni AFP.

Forum

XS
SM
MD
LG