Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 11:52

Mwanadiplomasia aliyebobea Lambert ateuliwa kusimamia sera ya China


Mark Lambert
Mark Lambert

Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imemteua  mwanadiplomasia aliyebobea Mark Lambert kuwa ni afisa mwandamizi wa masuala ya sera ya China, vyanzo vitano  vya habari vinavyofahamu suala hilo vimesema.

Uteuzi huu unaleta aina mpya ya uongozi kwa sehemu ya wizara hiyo ambayo imekuwa inakabiliwa na tatizo la wafanyakazi na ukosoaji kwa kwa jinsi navyoshughulikia juhudi mbalimbali zinazo husiana na China.

Kuna uwezekano kuwa Lambert akatajwa kuwa naibu waziri mdogo kwa masuala ya China na Taiwan, vyanzo hivyo vimeeleza, akijaza nafasi iliyoachwa wazi mwezi Juni na Rick Waters.

Waters aliwahi kuhudumu katika nafasi ya mkuu wa ofisi ya Uratibu wa China – maarufu kama “China House” – kitengo ambacho wizara ilikiunda mwishoni mwa mwaka 2022 kuunganisha sera mbalimbali za China kote katika kanda na masuala mbalimbali.

Iwapo Lambert atapachiwa cheo cha mratibu wa China House bado linajadiliwa hilo, vyanzo hivyo vilisema.

Uteuzi wa Lambert inavyoelekea hautabadilisha msimamo wa Washington kuhusu sera za China, ambazo uongozi wa Rais Joe Biden unasema ni moja ya sera zenye “ushindani mkubwa” wakati akiendelea kujaribu kuongeza mawasiliano na Beijing ili kuimarisha uhusiano.

Lakini Lambert, mwanadiplomasia anaye heshimika na mwenye uzoefu wa Asia Mashariki, bila shaka ataweza kuleta mabadiliko.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la Reuters.

Forum

XS
SM
MD
LG