Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 06, 2024 Local time: 04:42

Ufilipino na Australia zafanya mazoezi ya pamoja karibu na eneo la bahari ya South China Sea


Mazoezi ya kijeshi ya pamoja kati ya Australia na Ufilipino.
Mazoezi ya kijeshi ya pamoja kati ya Australia na Ufilipino.

Majeshi ya Australia na Ufilipino yamefanya mazoezi ya pamoja Ijumaa karibu na eneo lenye mgogoro la bahari ya South China Sea linalodaiwa kumilikiwa na China. Rais wa Ufilipino Ferdinand Marcos ameyapongeza kuwa ni “muhimu sana” katika mfano wa ushirikiano wa karibu.

China imepeleka mamia ya walinzi wa pwani, jeshi la majini na vyombo vingine kufanya doria na kutengeneza mazingira ya kijeshi katika bahari ya South China Sea, ambayo inadai kuwa yote ni milki yake licha ya uamuzi wa kimataifa ukieleza msimamo wake hauna msingi wa kisheria.

Mazoezi ya pamoja ya Ijumaa yalifanyika katika kituo cha jeshi la majini takriban kilomita 240 mashariki mwa Scarborough Shoal, eneo lenye utajiri wa uvuvi ambalo China ililichukua kutoka kwa Wafilipino mwaka 2012 baada ya mvutano mkali.

“Ukizingatia kuwa kumekuwepo matukio mengi yanayothibitisha hatari iliyoko katika eneo hilo, aina hii ya mazoezi, aina hii ya ushirikiano wa kimkakati wa karibu kati ya nchi hizo zilizoko katika kanda hiyo ni jambo muhimu kabisa,” Marcos aliwaambia waandishi.

“Ni sehemu muhimu ya jinsi tunavyo jiandaa kwa tukio lolote,” alieleza kuhusu mazoezi hayo, ambayo amesema waliyashuhudia yeye na Waziri wa Ulinzi wa Australia Richard Marles.

Mazoezi hayo ya anga, baharini na ardhini, ni mazoezi ya kwanza makubwa ya pamoja kwa nchi hizo mbili, ikifanya mazoezi ya majaribio ya mfano wa kukirejesha kisiwa kilichovamiwa na adui.

Kiasi cha wanajeshi 1,200 wa Australia na wanajeshi wa majini 560 wa Ufilipino walimimika katika ufukwe wakati wa mazoezi hayo, wakiwasili katika magari ya mashambulizi, kwa miamvuli na wengine katika ndege ya Osprey ya Marekani.

Ndege mbili za kivita aina ya F-35 za Australia zilitoa msaada wa anga, na meli za kivita za Australia zililinda himaya ya eneo lililozungungukwa na maji.

“Tuna nia ya dhati kwa dhana ya ulimwengu ambako migogoro inatatuliwa kwa kutumia sheria za kimataifa, na kile tutakacho fanya ni kuleta pamoja nguvu zetu za kijeshi kuimarisha utaratibu wenye kufuata kanuni,” Marles alisema katika mkutano wa waandishi wa habari baadae.

“Amani inaweza kupatikana kwa njia ya kulinda utaratibu wa kimataifa wenye kuzingatia kanuni.”

Marles na mwenzake wa Ufilipino Gilberto Teodoro pia wametoa taarifa ya pamoja Ijumaa ikieleza dhamira yao ya kupanga “doria za pamoja ya pande mbili katika bahari ya South China Sea… na maeneo mengine yenye maslahi ya pamoja.”

Forum

XS
SM
MD
LG