Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 08:44

China imetoa waraka mpya kuhusu maandalizi ya jeshi lake kushambulia Taiwan


Wanajeshi wa Jeshi la Ukombozi wa Wananchi wa China (PLA) wakitoka katika gwaride wakati wa sherehe za ufunguzi wa Bunge la 20 la Chama tawala cha Kikomunisti cha China mjini Beijing, China, Oktoba 16, 2022.
Wanajeshi wa Jeshi la Ukombozi wa Wananchi wa China (PLA) wakitoka katika gwaride wakati wa sherehe za ufunguzi wa Bunge la 20 la Chama tawala cha Kikomunisti cha China mjini Beijing, China, Oktoba 16, 2022.

Katika kuadhimisha miaka 96 ya Jeshi la Ukombozi wa Watu wa China CCTV maonyesha  mazoezi ya kijeshi na ushuhuda wa darzeni ya askari ambapo kadhaa wanaelezea nia yao ya kutoa maisha yao katika shambulio linalowezekana dhidi ya Taiwan.

China imetoa waraka mpya kuhusu maandalizi ya jeshi kuishambulia Taiwan na kuwaonyesha wanajeshi walioahidi kutoa maisha yao ikiwa itahitajika huku Beijing ikiendelea kuzidisha matamshi yake dhidi ya kisiwa hicho kinachojitawala.

Chasing Dreams filam ya sehemu 8 iliyorushwa hewani na shirika la utangazaji la serikali CCTV mapema wiki hii kuadhimisha miaka 96 ya Jeshi la Ukombozi wa Watu wa China inaonyesha mazoezi ya kijeshi na ushuhuda wa darzeni ya askari ambapo kadhaa wanaelezea nia yao ya kutoa maisha yao katika shambulio linalowezekana dhidi ya Taiwan.

Vyombo vya habari vya serikali na Jeshi la China - PLA mara nyingi hutoa nyenzo za propaganda zinazokuza uboreshaji wa jeshi na video maridadi za mazoezi ya kijeshi. China inadai Taiwan kisiwa chenye demokrasia kinachojitawala kama eneo lake na kutekwa kwa nguvu ikibidi.

Forum

XS
SM
MD
LG