Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 16:32

Papua New Guinea yaeleza faida za kuongezeka ushirikiano wa kijeshi na usalama kati yake na Marekani


Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd J. Austin akisalimiana na Waziri Mkuu wa Papua New Guinea James Marape huko Port Moresby, Papua New Guinea, Julai 27, 2023.
Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd J. Austin akisalimiana na Waziri Mkuu wa Papua New Guinea James Marape huko Port Moresby, Papua New Guinea, Julai 27, 2023.

Uongozi wa  Papua New Guinea unaahidi “kusambaza” faida za kuongezeka ushirikiano wa kijeshi na usalama na Marekani kufuatia ziara ya kwanza ya waziri wa ulinzi wa Marekani, wakati wakipuuza kuwepo hatari yoyote katika ushirikiano wa karibu wa nchi hiyo na China.

Waziri Mkuu James Marape Alhamisi aliupongeza Mkataba wa Ushirikiano wa Ulinzi wa PNG na Marekani, uliosainiwa Mei, akikubaliana na tathmini ya maafisa waandamizi wa wizara ya ulinzi ya Marekani kuwa Bunge la Taifa la nchi yake litaidhinisha makubaliano katika muda mfupi.

Pia alipongeza mkataba wa pembeni unaoitwa shiprider ambao utawaruhusu wanajeshi wa PNG kupanda meli za Ulinzi wa Pwani za Marekani katika kusaidia kulinda haki za uvuvi za nchi hiyo.

“Shughuli hiyo inaanza sasa,” Marape alisema, akiwa pembeni ya Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin kufuatia mkutano wao huko Port Moresby.

“Uwezo wetu wa ulinzi lazima uimarishwe,” alisema. “Ni ushirikiano wa hiari tulioufanya kuhusiana na ushirikiano wetu wa ulinzi lakini bila shaka kukiwa na faida zinazosambaa ambazo zinaunganisha uchumi [wetu] na, kingine muhimu, ni miundombinu muhimu ya kiuchumi.”

Maafisa wa PNG na Marekani walisema Alhamisi kuwa nchi zote mbili zimeanza kuangalia maeneo ambayo yanaweza kufanyika uwekezaji katika kuboresha miundombinu na utayari wa kijeshi.

Mkataba huo wa miaka 15 unatarajiwa pia kuwezesha uwepo mpana zaidi wa jeshi la Marekani katika kisiwa hicho na pia mazoezi ya pamoja, na uratibu mpana zaidi endapo kutakuwa na mgogoro wa kibinadamu.

Lakini Marape alisema jeshi la Marekani huko PNG litakuwa nchini humo kwa msingi wa kuja na kuondoka, nukta aliyoisisitiza Austin.

“Nataka kuweka wazi. Sisi hatutaki kuweka kituo cha kudumu hapa PNG,” Austin alisema.

“Tuna uhusiano wa muda mrefu na Papua New Guinea,” aliongeza.

“Lengo letu ni kuhakikisha tunaimarisha uwezo wa PNG kujilinda yenyewe na kulinda maslahi yake. … Sisi sote bila shaka tunaheshimu na kuthamini utaratibu wa kikanuni wa [ kimataifa].

Forum

XS
SM
MD
LG