Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 13:20

Marekani yaanza msukumo mpya kukabiliana na ushawishi wa China


Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin
Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin

Maafisa wakuu wa kijeshi wa Marekani na wanadiplomasia wiki hii wameanza msukumo mwingine wa pamoja, dhidi ya ushawishi wa China katika eneo la Indo-Pacific, wakitumai kupanua mikataba ya usalama, na mataifa muhimu ya Visiwa vya Pasifiki.

Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin Jumatano aliwasili mjini Port Moresby, nchini Papua New Guinea, kwa mfululizo wa mikutano na waziri mkuu wa nchi hiyo, na maafisa waandamizi wa ulinzi.

Ziara ya Austin nchini humo, ya kwanza kufanywa na waziri wa ulinzi wa Marekani aliye afisini, inakuja miezi michache tu baada ya nchi hizo mbili kutia saini Mkataba wa Ushirikiano wa Ulinzi, uliokusudiwa kutumika kama mfumo, wa kuimarisha uwezo wa vikosi vya ulinzi vya Port Moresby, na kuanzisha uwepo wa jeshi la Marekani - na vikosi vya mzunguko - kwenye kisiwa hicho.

Kutoka hapo, Austin anatazamiwa kusafiri hadi Brisbane, Australia kwa mkutano wa mashauriano, wa 33, wa Mawaziri wa Australia na Marekani (AUSMIN), ambapo ataungana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken, na wenzao wa Australia.

Blinken atawasili Australia baada ya kutembelea kisiwa cha Tonga, ambako alifungua ubalozi mpya wa Marekani, na pia kutembelea New Zealand.

Ziara za Austin na Blinken ni katia ya safari nyingine katika eneo hilo, za maafisa wa ngazi za juu wa Marekani.

Forum

XS
SM
MD
LG