Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 24, 2025 Local time: 00:02

Waziri wa ulinzi wa Marekani awataka washirika kutokuwa na hofu juu ya nyaraka zilizovuja


Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin
Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin

Waziri wa ulinzi wa Marekani Lloyd Austin alitaka leo kumalizwa kwa mzozo wowote kati ya Marekani na washirika wake kuhusu uvujaji mkubwa wa nyaraka za siri za Marekani.

Austin alizungumzia suala hilo alipokutana na viongozi wa ulinzi kutoka kote duniani nchini Ujerumani kujadili misaada zaidi ya kijeshi kwa Ukraine.

Waziri huyo alikiri kwamba mataifa mengine yamefuatilia kwa karibu suala hilo, Austin alilizungumzia mwanzo kabisa suala hilo katika hotuba yake ya ufunguzi wa Mkutano huo.

Hatua hiyo ilisisitiza uzito wa hali hiyo kwa kuwa nyaraka nyingi zilizosambazwa mtandaoni zilifichua maelezo kuhusu hali ya ndani ya vita nchini Ukraine na utoaji wa silaha unaendelea na vifaa vingine kwa ajili ya vikosi vya Ukraine vitani, masuala ya kijasusi ambayo maafisa wengine wa ulinzi wanahusika sana.

Austin alizungumza hayo katika siku ndefu ya Mkutano huo kwenye kituo cha kijeshi cha Ramstein nchini Ujerumani.

XS
SM
MD
LG