Papua New Guinea iliyopo kaskazini mwa Australia inafanya eneo hilo kuwa muhimu kimkakati. Ilikuwa ni eneo la vita vikali wakati wa vita vya pili vya dunia na ikiwa na idadi ya watu takriban milioni 10 ni taifa la kisiwa maarufu katika pacific.
Wizara ya mambo ya nje imesema makubaliano mapya yatatoa muundo wa kazi ambazo utasaidia kuboresha ushirikiano wa ushrikiano wa usalama , kuongeza uwezo wa vikosi vya usalama vya Papua New Guinea na kuongeza uthabiti katika eneo. maelezo yote ya makubaliano yatatolewa kwa umma mara baada ya wanasiasa wa pande zote kuwa na fursa ya kuchangia, katika miezi michache ijayo.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken aliwaambia waandishi wa habari kwamba nchi yake itakuwa wazi kabisa.
Marekani imeongeza mwelekeo wake katika pacific , ikifungua balozi katika visiwa vya Solomon na Tonga pamoja na kufufua tena ushirikiano wa kujitolea wa peace corps, na kuhimiza uwekezaji zaidi wa biashara.