Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 03:55

Australia inataka Assange kuachiliwa huru


Mwanzilishi wa shirika la habari la upekuzi la WikiLeaks Julian Assange akizungumza nje ya ubalozi wa Ecuador, mjini London, Feb 5, 2016 PICHA: REUTERS
Mwanzilishi wa shirika la habari la upekuzi la WikiLeaks Julian Assange akizungumza nje ya ubalozi wa Ecuador, mjini London, Feb 5, 2016 PICHA: REUTERS

Waziri mkuu wa Australia Anthony Albanese amesema kwamba hafurahishwi na hatua ya kuendelea kuzuiliwa kwa Julian Assange, mwanzilishi wa mtandao wa Wikileaks, huko nchini Uingereza.

Assange anasubiri uamuzi wa mahakama kutokana na ombi la Marekani kutaka akabidhiwe kwa Marekani.

Akizungumza katika mahojiano na shirika la habari la serikali ya Australia mjini London, waziri mkuu wa Australia Anthony Albanese amesema kwamba inatosha kuendelea kumshikilia Assange na kwamba swala hilo huenda litatatuliwa kabla ya rais wa Marekani Joe Biden kuitembelea Australia baadaye mwezi huu wakati wa mkutano wa viongozi wa Quad 2023 utakaohudhuria pia na waziri mkuu wa India Narendra Modi na kiongozi wa Japan Kishida Fumio.

Assange, mzaliwa wa Australia anatakiwa nchini Marekani kawa shutuma za kuvujisha nyaraka za siri za kijeshi na diplomasi kati yam waka 2010 na 2011.

Marekani inasema kwamba alivunja sheria na kuhatarisha Maisha.

XS
SM
MD
LG