Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 23:35

Sakata la deni la taifa la Marekani lazingira ziara ya rais Biden


Biden
Biden

Huku rais Joe Biden, wa Marekani, na viongozi wa bunge wakiendelea na mazungumzo kujadili suala la kuongeza kiwango cha deni ili kuifanya Marekani kutokiuka majukumu yake, mivutano ya  miezi kadhaa bado inaweza kuvuruga mikutano ya kiongozi wa Marekani na washirika wake nchini Japan na Australia.

Rais Biden anatarajiwa kuondoka Washington kuelekea Hiroshima kuhudhuria mkutano wa kundi la viongozi wa mataifa saba tajiri yaani G7 siku ya Jumatano, siku moja baada ya mkutano wake wa pili wa ukomo wa deni na viongozi wa bunge.

Mei 22, rais Biden ataelekea Sydney kwa mkutano wa Quad atasimama kwa muda mfupi huko Port Moresby, Papua New Guinea, kukutana na viongozi wa umoja wa visiwa vya Pasifiki.

Mikutano hiyo imeelezewa kama fursa ya kuimarisha ushirikiano kwa changamoto za kikanda na kuendeleza maslahi ya kimkakati ya Marekani katika kukabiliana na ushawishi wa China.

XS
SM
MD
LG