Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 03:33

Ufilipino imesema itafanya kazi kuondoa kizuizi ambacho China ilikiweka


Mzozo wa Ufilipino na China katika South China Sea
Mzozo wa Ufilipino na China katika South China Sea

Walinzi wa pwani ya Ufilipino wamesema kizuizi hicho ambacho kiliwekwa Ijumaa katika eneo la Scarborough Shoal kinawanyima wavuvi wa Ufilipino riziki yao.

Ufilipino imesema leo Jumatatu kwamba itafanya kazi kuondoa kizuizi kinachoelea ambacho China ilikiweka ili kuzuia meli za uvuvi za Ufilipino kwenye eneo linalozozaniwa la South China Sea.

“Kuwekwa na Jamhuri ya Watu wa China kizuizi kinakiuka haki za uvuvi wa jadi za wavuvi wetu,” Mshauri wa Usalama wa Taifa wa Ufilipino Eduardo Ano alisema katika taarifa. Walinzi wa pwani ya Ufilipino wamesema kizuizi hicho ambacho kiliwekwa Ijumaa katika eneo la Scarborough Shoal kinawanyima wavuvi wa Ufilipino riziki yao.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China, Wang Wenbin amesema maji hayo yanayozozaniwa ni ardhi ya China. China ilichukua udhibiti wa eneo la Scarborough Shoal kutoka Ufilipino mwaka 2012 na kudai uhuru juu ya sehemu kubwa yenye utajiri katika South China Sea.

Madai yanayoshindaniwa yanajumuisha yale kutoka Brunei, Malaysia, Ufilipino, Taiwan na Vietnam.

Forum

XS
SM
MD
LG