Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 19:05

Bill Gates na Jeff Bezos kuunga mkono uchimbaji wa madini Zambia


Mkurugenzi Mtendaji wa Amazon Jeff Bezos (kushoto) akiongea na Mkurugenzi Mtendaji wa Microsoft Bill Gates huko New York 31 Mei, 2001. Picha na STAN HONDA / AFP
Mkurugenzi Mtendaji wa Amazon Jeff Bezos (kushoto) akiongea na Mkurugenzi Mtendaji wa Microsoft Bill Gates huko New York 31 Mei, 2001. Picha na STAN HONDA / AFP

KoBold Metals kampuni yenye makao yake California, nchini Marekani inayoungwa mkono na mabilionea Bill Gates na Jeff Bezos, ilisema inalenga kuanzisha mradi wa uzalishaji shaba na kobalti nchini Zambia katika kipindi cha miaka kumi.

KoBold inatumia takriban dola milioni 150 kuchochea utafutaji wake wa madini zaidi katika mradi wa Mingomba, ulioko kwenye ukanda mashuhuri wa shaba katika bara la Afrika.

Utafiti wa ziada utakamilika mwaka 2024, alisema Mfikeyi Makayi, Mkurugenzi Mtendaji wa mradi huo wa Silicon Valley nchini Zambia . "Ni mradi wa kuvutia sana na tumesema ndani ya muongo mmoja tungetaka Mingomba kuwa mgodi unaozalisha,” Makayi aliliambia shirika la habari la Reuters.

Kampuni ya KoBold hutumia akili bandia kutafuta shaba, kobalti, nikeli na lithiamu madini yanayohitajika duniani kwa nishati safi na kuharakisha ukuaji katika utengenezaji wa magari ya umeme.

Marekani inatafuta vyanzo mbadala vya upatikanaji wa madini muhimu na ufadhili kutoka kwa wawekezaji wa Marekani wameiwezesha KoBold kuongeza utafutaji, Makayi sema.

KoBold inataka kupata machimbo mengi zaidi kutoka katika mgodi mikubwa kama wa Mingomba nchini Zambia na pia itatafuta fursa nchini Botswana, Namibia na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, alisema Makayi
Kampuni ya KoBold pia hutafuta madini muhimu ya chuma na makampuni ya BHP Group na Rio Tinto katika miradi iliyoko Australia.

Forum

XS
SM
MD
LG