Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 15:31

Chama tawala cha ANC Afrika Kusini chapoteza zaidi ya nusu ya wanachama


Rais wa Chama tawala cha African National Congress (ANC) Cyril Ramaphosa akiwahutubia wafuasi wake katika uwanja wa Dobsonville huko Soweto Septemba 3, 2023. Picha na Phill Magakoe / AFP.
Rais wa Chama tawala cha African National Congress (ANC) Cyril Ramaphosa akiwahutubia wafuasi wake katika uwanja wa Dobsonville huko Soweto Septemba 3, 2023. Picha na Phill Magakoe / AFP.

Uungwaji mkono kwa chama tawala cha Afrika Kusini cha African National Congress (ANC), kilichokuwa madarakani tangu mwaka 1994, umepungua hadi chini ya asilimia 50 kabla ya uchaguzi mkuu kufanyika mwakani, kulingana na kura mpya ya maoni.

Chama kilichowahi kuongozwa na Nelson Mandela huenda kikapata asilimia 45 ya kura mwakani, dhidi ya asilimia 31 ya chama cha Democratic Alliance (DA), chama kikuu cha upinzani, kulingana na kura ya maoni ya Taasisi ya Utafiti wa Jamii (SRF).

Matokeo kama haya yanaweza kukifanya chama tawala kupoteza wingi wake bungeni.

"Takwimu zinaonyesha kuwa kiwango cha wanaokiunga mkono chama cha ANC kinaonekana kupungua kwa kiasi fulani," ilisema ripoti hiyo ya SRF.

Uungwaji mkono kwa ANC umepungua kutoka asilimia 52 mwezi Machi kulingana na kura ya maoni, ambazo zinatokana na mahojiano na wawakilishi zaidi ya 1,400 waliojiandikisha "kijiografia na kidemografia" mwezi Oktoba.

Wafuasi wa Chama tawala cha Afrika Kusini huko Soweto Septemba 3, 2023. Picha na Phill Magakoe / AFP
Wafuasi wa Chama tawala cha Afrika Kusini huko Soweto Septemba 3, 2023. Picha na Phill Magakoe / AFP

Uungwaji mkono wa chama cha upinzani cha DA umeongezeka kutoka asilimia 24 katika kipindi kama hicho.

Kama uchaguzi ungefanyika kesho, chama cha tatu kwa ukubwa Afrika Kusini, cha mrengo wa kushoto cha Economic Freedom Fighters (EFF) kingepata takriban asilimia tisa ya upendeleo, kulingana na utafiti uliofanywa na Taasisi ya Afrika Kusini.

Mapema wiki hii, tume ya uchaguzi ya Afrika Kusini ilisema uchaguzi utafanyika kati ya mwezi Mei na Agosti mwakani.

Taswira ya ANC imeharibika na kuchafuliwa na ufisadi, urafiki na rekodi duni ya kiuchumi.

Chama cha ANC hakijawahi kupata chini ya asilimia 50 ya kura katika uchaguzi wa kitaifa tangu kurejea kwa demokrasia miongo mitatu iliyopita.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AFP

Forum

XS
SM
MD
LG