Uchunguzi ulifunguliwa siku ya Alhamisi uliopewa mamlaka ya kubaini jukumu kwenye moto huko Johannesburg ambao ulisababisha vifo vya watu 77, na kuangazia magenge ambayo yanateka majengo yaliyotelekezwa katikati ya jiji na kuyakodisha kinyume cha sheria.
Moja ya maafa mabaya sana kutokea katika kumbukumbu ya maisha katika kitovu cha uchumi wa Afrika Kusini, moto huo ambao ulizuka Agosti 31 katika jengo bovu lililojaa wahamiaji wa kigeni. Waathiriwa wengi walichomwa kiasi cha kutotambulika.
Wakazi walisema wakati wa maafa jengo hilo lilikuwa limechukuliwa na vikundi vya wahalifu ambavyo huwatoza kodi wakazi na kuwanyonya lakini pia kutoa makazi ya bei nafuu kwa wale ambao wanaweza kubaki bila makazi.
Wakazi wa majengo kama hayo pia hutegemea kuunganishiwa umeme kinyume cha sheria, majiko ya gesi na wakati umeme ukikatika nchini humo hutumia mishumaa ambayo yote ni hatari sana ya kusababisha moto kuzuka.
Forum