Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 01, 2024 Local time: 14:05

Mdahalo wa CNN watoa fursa kwa Trump na Biden kuwashawishi wapiga kura zaidi


Picha hizi za Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump, kushoto, Rais wa Marekani Joe Biden wakati wa mdahalo wa CNN wa wagombea urais ulioandaliwa na CNN, Juni 27, 2024, in Atlanta.
Picha hizi za Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump, kushoto, Rais wa Marekani Joe Biden wakati wa mdahalo wa CNN wa wagombea urais ulioandaliwa na CNN, Juni 27, 2024, in Atlanta.

Rais wa Marekani Joe Biden na Rais wa zamani wa Marekani na mgombea urais kwa tiketi ya chama cha Republikan Donald Trump wakishiriki katika mdahalo wa CNN wa wagombea urais wa uchaguzi wa mwaka 2024 katika studio za Kituo cha Televisheni cha CNN huko Atlanta, Georgia, Juni 27, 2024.

Mdahalo huu ni fursa kwa wagombea wote wawili kujaribu kutengeneza tena maelezo ya kisiasa na kuwashawishi wapiga kura waliokuwa hawana uamuzi wampe nani kura zao.

Biden, mdemokratiki aliyeko madarakani, ana fursa ya kuwahakikishia wapiga kura tena kuwa, akiwa na umri wa miaka 81, anauwezo wa kuiongoza Marekani kukabiliana na changamoto kadhaa.

Wakati huohuo, Trump mwenye umri wa miaka 78 anaweza kutumia fursa hiyo kujaribu kuonyesha kukutwa na makosa ya uhalifu New York hakumshughulishi na kuwashawishi mamilioni ya watu kuwa anasifa za kuweza kurejea tena Ikulu kuongoza nchi.

Mdahalo wa Alhamisi huko Atlanta utaweka rikodi kwa kuongoza kwa mara ya kwanza – haikuwahi kutokea huko nyuma wagombea wawili wanao wania kuingia White House wakikabiliana katika umri mkubwa, na kabla ya hapo haijawahi kutokea CNN ⁣⁣kuwa wenyeji wa mdahalo wa uchaguzi mkuu wa rais

Chanzo cha habari hii ni CNN

Forum

XS
SM
MD
LG