Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 18:38

Trump alenga kuhusu uhamiaji na kutishia vikwazo kwa nchi kadhaa


Rais wa zamani akiwa katika kampeni.
Rais wa zamani akiwa katika kampeni.

Mgombea urais wa Marekani Donald Trump amerejea kwenye kampeni baada ya kukutwa na hatia huko New York kwa kugushi rekodi za biashara.

Rais wa Marekani Joe Biden
Rais wa Marekani Joe Biden

Katika mikutano aliyoifanya Magharibi mwa Marekani, Trump alilenga kuhusu uhamiaji na kutishia vikwazo kwa nchi kadhaa, ikiwemo China kama hawatawazuia watu kuondoka kuja Marekani.

Donald Trump alirejea kwenye kampeni ya urais wiki iliyopita huko Arizona, ambako alisema Rais Joe Biden amepoteza udhibiti wa mpaka wa Marekani na Mexico.

Donald Trump, Mgombea Urais wa Republican anasema: “Yote hayo si endelevu. Lakini uvamizi wa Biden siyo ajali. Ni hatua ya makusudi ya kuharibu utaifa wetu na mipaka yetu. Kwa namna fulani, kuna mtu atajieleza kwanini wametaka hili litokee. Nahisi ni kwasababu ya kura.”

Rais wa zamani Donald Trump (kushoto) na Rais wa Marekani Joe Biden
Rais wa zamani Donald Trump (kushoto) na Rais wa Marekani Joe Biden

Hakuna ushahidi kwamba kuna raia ambao si wa Marekani wanapiga kura kwa idadi kubwa katika uchaguzi wa Marekani.

Trump azliulizwa jinsi ya kusitisha uhamiaji haramu na kusema atachukua hatua dhidi ya serikali za kigeni ambazo zichangia katika hilo.

Donald Trump, Mgombea Urais wa Republican anaeleza: “Kama China au baadhi ya nchi nyingine zitakuwa na tabia hii mbaya, tuna vitu ambavyo tunaviita ushuru ambavyo ni vikali sana.”

Utawala wa Biden mwezi huu ulichukua hatua ya kuzuia maombi ya hifadhi katika mpaka wa Mexico wakati ukamataji wa wanaovuka mpaka kinyume cha sheria utavuka 2,500 kwa siku.

Biden anasema mageuzi ya uhamiaji ni muhimu hahaitaji kuja na matamshi ya uchochezi ambayo Trump anayelekeza kwa wahamiaji.

Rais Joe Biden amesema: “Wakati tunapambana kuwa na mageuzi ya msingi ya uhamiaji, anawaita wahamiaji wabakaji na wauaji. Anasema wao si watu. Anasema wahamiaji kwa maneno yake ‘damu yenye sumu kwa nchi yetu’. Jamani, mlionitangulia mnaitaka nchi iwe kwa baadhi yet utu. Tunataka iwe nchi ya sisi wote.”

Biden anasema matamshi ya Trump dhidi ya uhamiaji yamevuka mpaka wa misingi ya waanzilishi wa Marekani.

Rais Joe Biden alieleza kuwa: “Unawakilisha sisi tulivyo kama taifa la wahamiaji, taifa la wenye ndogo, taofa lenye uhuru. Hivyo Marekani tunayoshirikiana.”

Mikutano ya Trump wiki iliyopita ilikuwa ya kwanza tangu alipokutwa na hatia ya kugushi rekodi za biashara ili kuficha malipo ya siri kabla ya uchaguzi wa mwaka 2016.

Aliuambia mkutano huko Nevada kwamba kesi yake ilikuwa ni matokeo ya Biden kutumia ‘silaha’ hiyo ya mfumo wa sheria wakati akishindwa katika suala la mpaka.

Donald Trump, Mgombea Urais wa Republican anasema: “Huu ni mpaka mbaya sana katika historia ya dunia. Hakuna nchi ya dunia ya tatu inatumia silaha pale ambapo wanawafuatilia wagombea wa kisiasa kama tunavyofanya sisi.”

Ukusanyaji maoni wa Associated Press mwezi Machi umeonyesha mabadiliko ya mwenendo wa wapiga kura kuhusu uhamiaji, huku karibu theluthi moja ya Wamarekani hivi sasa wanasema ni hatari kubwa kwa vile wahamiaji wanafanya uhalifu. Hiyo ikiwa juu kutoka asilimia 19 ambao walifikiria hivyo mwaka 2017.

Forum

XS
SM
MD
LG