Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 19:17

Trump asema atakata rufaa kutokana na maamuzi ya kukutwa na hatia


FILE PHOTO: Rais wa zamani Donald Trump
FILE PHOTO: Rais wa zamani Donald Trump

Mgombea Urais wa Marekani, Donald Trump anasema atakata rufaa kutokana na maamuzi ya kukutwa na hatia ya uhalifu kwa kugushi rekodi za biashara kabla ya uchaguzi wa 2016.

Mwandishi wa VOA Scott Stearns anaangazia matarajio ya rais wa zamani katika rufaa yake na iwapo hatia hiyo huenda ikabadilisha kabla ya siku ya uchaguzi.

Donald Trump anasema alikosewa kwenye mahakama ya New York wiki iliyopita na jaji ambaye alitoa fursa nyingi kwa yeye kukata rufaa.

Donald Trump, Mgombea Urais wa Republican: “Kwahiyo, tutakata rufaa kwa kashfa hii. Tutakwenda kukata rufaa kuhusu mambo mengi. Hakuturuhusu sisi kuwa na mashahidi. Hakuturuhusu kuzungumza. Hakuturusu sisi kufanya chochote. Jaji alikuwa dhalimu.”

Trump alikutwa na hatia kwa makosa 34 ya kugushi rekodi ya biashara ili kuficha malipo yaliyotumika kinyume cha sheria ili kushawishi uchaguzi wa mwaka 2016 alioshiriki. Trump anasema kesi “iliibwa” na wale wanaomuunga mkono Rais Joe Biden.

Biden anasema hatia ya Trump inathibitisha tena kwamba hakuna mtu ambaye yuko juu ya sheria.

Rais wa Marekani Donald Trump
Rais wa Marekani Donald Trump

Rais Joe Biden anasema: “Sasa atapewa fursa, kama inavyotakiwa, kukata rufaa kwa uamuzi uliochukuliwa kama inavyokuwa kwa kila mtu ambaye anakuta na fursa kama hiyo. Hivi ndivyo mfumo wa sheria wa Marekani unavyofanya kazi. Ni kutojali, ni hatari sana, ni kutowajibika kwa mtu yeyote kusema kuwa kulikuwa na wizi kwasababu tu hakutaka maamuzi yaende na kinyume alivyotaka yeye.”

Kuhusu rufaa, mawakili wa Trump huenda wakaanza na kuangalia kama sheria iliyotumiwa kumshtaki ilikuwa isyoeleweka kabisa, anasema profesa wa sheria huko Georgetown, Abbe Smith.

Abbe Smith, Georgetown: “Je sheria yenyewe ili pana au haieleweki kiasi kwamba huenda ilikuwa na mapungufu, na watu wakajikuta katika wakiwemo katika mapungufu hayo ambayo hawakujua hasa nini walikuwa wanakabiliana nacho, hawakuelewa sheria inakataza nini na sheria inaruhusu nini, hasa kutokana na maelezo ya sheria.”

Smith anasema mawakili wa Trump huenda wakaangalia kama jaji katika kesi aliruhusu ushahidi ambao haikutakiwa uwemo au alizuia ushahidi wa upande wa utetezi ambao alitakiwa auruhusu.

Donald Trump, Mgombea Urais wa Republican: “Wakati tulipokuwa tunataka kufanya mambo, hakuturuhusu, hakuturuhusu tufanye mambo hayo. Lakini wakati serikali ilipotaka kitu, walipata kila walichotaka. Walipata kila kitu.”

Trump huenda pia atakata rufaa katika misingi ya shauri lenyewe halikuwa na uzito.

Abbe Smith, Chuo cha Sheria, Georgetown: “Na hapo nadhani, pengine upande wa utetezi ulishindwa kupinga ushahidi wa Stormy Daniels ukipendekeza kwamba mahusiano ya kimapenzi kati yake na Bwana Trump yalikuwa ni kitu cha kuridhiana, huenda kuna misingi yenye nguvu ya kukata rufaa kuhusu ufanisi wa kesi iliyvoendeshwa.”

Mikakati yoyote ile, Trump na mawakili wake huenda wasikate rufaa kabla ya Julai 11 wakati hukumu itakapotolewa, anasema David Shapiro, wa chuo cha masuala ya sheria ya uhalifu cha John Jay.

David Shapiro, Chuo cha Sheria ya Uhalifu, John Jay: “Kuna dalili atasubiri kuhukumiwa. Kwa njia hiyo yeye na mawakili wake, watakuwa na mtizamo kamili wa kitu gani kinamkabili, badala ya kufanya mambo kidogo kidogo, ambayo ni miongoni mwa mambo mengine, inakula rasilimali za fedha za Bwana Trump na kwa kweli hapati fursa nzuri ya kuongeza chochote katika kesi yake.”

Rufaa huenda isitolewa maamuzi kabla ya siku ya uchaguzi, anasema Smith.

Abbe Smith, Chuo cha Sheria, Georgetown: “Huu si mchakato wa haraka. Mimi sioni, hata kama idara ya Rufaa itaiona kesi hii ni maalum na ya haraka kwasababu ya uchaguzi wa rais. Bado sioni hilo likitokea kabla ya Novemba.”

Kama hatia haitabadilishwa kabla ya siku ya uchaguzi, Trump atakuwa mhalifu wa kwanza kusimama kuwania urais kwa tiketi cha chama kikubwa nchini Marekani.

Forum

XS
SM
MD
LG