Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Juni 26, 2024 Local time: 20:46

Trump anasema yuko tayari kukubali kifungo cha jela


Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump
Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump

Donald Trump amesema atakubali kifungo cha nyumbani au kifungo cha jela baada ya jopo la Mahakama ya New York kumkuta na hatia wiki iliyopita katika kesi ya kihistoria, lakini itakuwa vigumu kwa wananchi kukubali hilo.

“Sina uhakika kwamba wananchi watakubaliana na hilo, mgombea huyo wa urais kwa tiketi ya chama cha Repubican alikimbia kituo cha televisheni cha Fox News katika mahojiano yaliyopeperushwa Jumapili.

“Nadhani itakuwa vigumu kwa wananchi kulikubali hilo. Unajua, wakati fulani, kuna hatua ambayo haiwezi kuvumiliwa.”

Trump hakufafanua kile kinachoweza kutokea ikiwa hatua hiyo itachukuliwa. Hukumu yake inatarajiwa kusomwa tarehe 11 Julai, siku nne kabla ya Warepublican kukutana na kumteua rasmi mgombea wao wa urais kukabiliana na Rais Joe Biden katika uchaguzi wa Novemba.

Alipoulizwa ni nini wafuasi wa Trump watafanya ikiwa atafungwa jela, mwenyekiti mwenza wa Kamati ya Kitaifa ya chama cha Republican, Lara Trump aliiambia CNN: “Watafanya kile wamechokuwa wakifanya tangu mwanzo, kuwa watulivu na kudhihirisha upinzani wao kwenye sanduku la kura tarehe 5 Novemba. Hakuna jingine la kufanya isipokuwa kufanya sauti yao isikike kwa sauti kubwa na kwa uwazi na kupinga jambo hilo,” alisema.

Forum

XS
SM
MD
LG