Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Julai 03, 2024 Local time: 13:33

Chama cha siasa Marekani kinazungumzia hatia ya Donald Trump


Spika wa Baraza la Wawakilishi Mike Johnson wa chama cha Republican
Spika wa Baraza la Wawakilishi Mike Johnson wa chama cha Republican

Uamuzi wa jopo la majaji wa New York kumtia hatiani rais wa zamani unaonyesha hakuna mtu aliye juu ya sheria, inasema kampeni ya Biden

Hukumu ya kihistoria ya rais wa zamani wa Marekani Donald Trump katika mahakama ya New York nchini Marekani kwa makosa 34 ya uhalifu siku ya Alhamisi iliibua majibu tofauti kutoka kwa pande zote za kisiasa.

Kampeni ya mpinzani wa Trump katika uchaguzi, na mgombea urais wa chama cha Democratic, Rais Joe Biden, imesema uamuzi wa jopo la majaji wa New York kumtia hatiani rais wa zamani unaonyesha kuwa hakuna mtu aliye juu ya sheria.

“Donald Trump amekuwa akiamini kimakosa kuwa hatawajibishwa kwa kuvunja sheria kwa manufaa yake binafsi,” ilisema taarifa ya kampeni ya Biden na Harris. “Lakini maamuzi ya Alhamisi hayabadilishi ukweli kwamba watu wa Marekani wanakabiliwa na ukweli rahisi. Bado kuna njia moja tu ya kumzuia Donald Trump kuingia tena ofisi ya Oval katika White House, na ni kupitia sanduku la kura.”

Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump katika mahakama ya Manhattan mjini New York
Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump katika mahakama ya Manhattan mjini New York

Kampeni ya Trump ilidai katika taarifa kwamba haikutendewa haki kwenye kesi katika moja ya maeneo ya kiliberali katika taifa.

Wakati huo huo, Spika wa Baraza la Wawakilishi Mike Johnson, kiongozi wa ngazi ya juu wa Republican, alisema katika taarifa, “Leo ni siku ya aibu katika historia ya Marekani.

Wademocrat katika bunge walisema -- jopo la wanachama 12 -- limethibitisha nguvu ya mfumo wa kisheria Marekani.

Forum

XS
SM
MD
LG