Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 01, 2024 Local time: 14:10

Trump ashamiri kwenye TikTok siku chache baada ya kesi ya New York


Trump akitoa hotuba siku moja baada ya kupatikana na hatia ya uhalifu na jopo la mahakama ya New York. Ijumaa Mei 31, 2024.
Trump akitoa hotuba siku moja baada ya kupatikana na hatia ya uhalifu na jopo la mahakama ya New York. Ijumaa Mei 31, 2024.

Saa chache baada ya kujiunga na mtandao wa kijamii wa TikTok, mgombea urais wa Repablikan Marekani Donald Trump, tayari amejipatia zaidi ya wafuasi milioni 1 kwenye jukwaa hilo alilojaribu kulipiga marufuku wakati alipokuwa rais, kwa misingi ya kulinda usalama wa taifa.

Uamuzi wa kujiunga na TikTok huenda ukamsaidia Trump kuwafikia wapiga kura vijana, wakati anapojaribu kurejea White House kupitia uchaguzi wa Novemba 5, dhidi ya rais wa sasa Joe Biden.

Tayari timu ya kampeni ya Biden ipo kwenye TikTok, ingawa kiongozi huyo ametia saini mswaada unaolenga kupiga marufuku App hiyo inayotumiwa na takriban wamarekani milioni 170, iwapo mmiliki wake ByteDance kutoka China, hatokubali sehemu yake ya kiutawala iwepo Marekani.

Kampuni hiyo imepinga hatua hiyo mahakamani, ikihitajika kuuza tawi lake la Marekani kufikia Januari mwaka ujao, la sivyo TikTok ipigwe marufuku Marekani. Kampuni hiyo imesema kuwa kamwe haitatoa data za watumiaji wa Marekani kwa serikali ya China, na kwamba tayari imeweka mikakati inayozuia hilo kufanyika.

Forum

XS
SM
MD
LG