Ameshtakiwa kwa kughushi rekodi za fedha ili kuficha malipo aliyotoa kwa mwanamke mcheza filamu za ngono ili kushawishi matokeo ya ucahguzi ya mwaka 2016.
Aliendelea na kampeni ya uchguzi wa mwaka huu nje ya mahakama ya New York.
Kwa takriban wiki sita zilizopita, Donald Trump alilalamika kwamba mashtaka dhidi yake ni ya kisiasa.
Donald Trump, Mgombea Urais wa Republican anasema: “Haijawahi kutokea kitu kama hiki katika historia ya nchi yetu. Ni kashfa. Ni uingiliaji kati uchaguzi kwa kiwango ambacho hakijawahi kutokea hapo kabla.”
Kampeni ya Rais Joe Biden kwa kiasi kikubwa ilijizuia kutoa maoni kuhusu kesi ya mpinzani wake. Mpaka wiki hii…
… na kutoka katika kampeni ya Biden alijitokeza kwa muigizaji Robert De Niro nje ya mahakama.
Robert De Niro, Muigizaji: “Wakati Trump alipowania mwaka 2016, ilikuwa ni kama utani. Huyu mtu kweli anawania urais, ‘hapana, haiwezi kamwe kutoka.’ Tulisahahu mafunzo ya historia ambayo yametuonyesha kuna wenye vichekesho wengine ambao hawakuwa na nia ya dhati mpaka walipokuwa madikteta matata. Kwa Trump, tumepata nafasi ya pili na hakuna anayecheka hivi sasa.”
Mshauri wa Trump, Jason Miller anasema hiyo inaonyesha Trump alikuwa sahihi tangu mwanzo.
Jason Miller, Mshauri wa Trump: “Kwahiyo, kina Biden wameshakwisha. Baada ya miezi ya kusema kwamba siasa haina chochote kuhusu kesi hii, wamefika na kufanya kampeni hapa Manhattar siku ya kesi ya Rais Trump.”
De Niro anaelezea tangazo jipya kutoka kwa kampeni ya Biden linaloangazia maneno ya Trump, na nukuu “amezidi kuongeza kasi na kwa hatari sana ya kutaka madaraka tangu aliposhindwa uchaguzi wa 202.”
De Niro narration from campaign ad: “Sasa awania tena. Mara hii anatishia atakuwa dikteta, ataifuta katiba.”
Trump from campaign ad: “Kama sitachaguliwa, kutakuwa na umwagaji damu.”
De Niro narration from campaign ad: “Trump anataka kulipiza kisasi, na atahakikisha hakuna kitakachomzuia.”
Biden from campaign ad: “Mimi ni Joe Biden, naidhinisha ujumbe huu.”
Kampeni ya Trump inasema Biden anajaribu kuwavuruga wapiga kura kutokana na kushindwa kwake. Mesmaji Karoline Leavitt anasema.
Karoline Leavitt, Msemaji Kampeni ya Trump: “Kwasababu Joe Biden ni dhaifu. Anasikitisha. Ni tishio kwa demokrasia, siyo tu kwa silaha yake anayoitumia ya mfumo wa sheria lakini kwa uvamizi wake mpana wa mpakani ambao unaruhusu watu wengi kuingia nchini kinyume cha sheria – magaidi, wahalifu. Uchumi wetu uko katika hali mbaya. Tunaelekea katika vita vya tatu vya dunia. Hayo ni masuala ya kweli ambayo Wamarekani wanayajali.”
Ukusanyaji maoni uliofanywa na PBS News Hour na NPR na Marist unasema wapiga kura wa Marekani hawafuatilii kesi. Jopo la mahakama litaamua iwapo kumuchia Trumpa kama rais wa kwanza wa Marekani kushtakiwa kwa uhalifu au kumkuta na hatia ya uhalifu kwa rais anayewania kuchaguliwa.
Forum