Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 07:32

Trump apatikana na hatia kwa mashtaka 34 ya jinai


Rais wa zamani wa Marekani Donal Trump akitoka nje ya mahakama baada ya kupatikana na hatia ya uhalifu kwa mashtaka ya jinai 34.
Rais wa zamani wa Marekani Donal Trump akitoka nje ya mahakama baada ya kupatikana na hatia ya uhalifu kwa mashtaka ya jinai 34.

Jopo la wajumbe wa mahakama moja mjini New York, Alhamisi limempata na hatia rais wa zamani wa Marekani Donald Trump kwa mashtaka 34 ya kugushi hati zake za biashara.

Jopo la mahakama la wajumbe 12 lilitathmini na kutafakari kwa siku mbili ushahidi wote liliopokea na kutoa uamuzi dhidi ya Trump mwenye umri wa miaka 77 , katika kesi ya kwanza kabisa ya uhalifu dhidi ya rais wa zamani wa Marekani.

Wakili wa Trump, Todd Blance aliomba uamuzi huo wa kupatikana na hatia ubatilishwe, lakini hakimu wa Mahakama Kuu ya New York Joan Merchan mara moja alipinga hoja hiyo.

Trump alipatikana na hatia kutokana na mashtaka kwamba alimlipa Stormy Daniels, mwanamke muigizaji wa filamu za ngono karibu dola 130, 000 ili kumnyamazisha, inayofahamika kama "hush money" kabla ya uchaguzi mkuu wa 2016.

Hukumu ya Trump imepangwa kutolewa Julai 11, kati kati ya kampeni yake ya kujaribu kurudi kwenye White House, siku chache tu kabla ya kuanza kwa Kongamano la Kitaifa la chama cha Republican hapo Julai 15.

Trump bado anatarajiwa kugombania kiti cha rais wakati wa uchaguzi wa mwezio Novemba dhidi ya Rais Joe Biden aliyemshinda wakati wa uchaguzi wa 2020.

Picha ya kuchorwa inaonyesha hali ilivyokuwa wakati wa hoja za mwisho mwisho katika kesi ya Trump.
Picha ya kuchorwa inaonyesha hali ilivyokuwa wakati wa hoja za mwisho mwisho katika kesi ya Trump.

Uteuzi wake kugombania kiti cha rais kwa niaba ya chama hicho unatarajiwa kuidhinishwa rasmi wakati wa kongamano hilo.

Hatia ya kihistoria imepata majibu ya haraka kutoka kila nyanja ya kisiasa.

Kampeni ya uchaguzi ya mpinzani wa Trump na mgombea urais wa Democratic, Rais Joe Biden, amesema kuwa uamuzi wa jopo la mahakama huko New York kumkuta rais wa zamani na hatia kumeonyesha kuwa hakuna mtu ambaye yuko juu ya sheria.

“Donald Trump siku zote amekuwa akifanya makosa kuamini kuwa kamwe hatakabiliwa na matokeo kwa kuvunja sheria kwa ajili ya manufaa yake binafsi,” kampeni ya Biden na Harris imesema katika taarifa. “Lakini hatia ya leo haibadilishi ukweli kwamba watu wa Marekani wana ukweli rahisi. Bado kuna njia moja ya kumuweka Donald Trump nje ya ofisi ya Oval: nayo ni boksi la kura.”.

Kampeni ya Trump imedai katika taarifa yake kwamba hakuweza kupata kesi ya haki katika moja ya maeneo ya waliberali zaidi katika taifa hili.

Waandamanaji nje ya mahakama ya New York baada ya Trump kupatikana na hatia. Mei 30, 2024.
Waandamanaji nje ya mahakama ya New York baada ya Trump kupatikana na hatia. Mei 30, 2024.

“Hii ilikuwa ni fedheha. Hii ilikuwa kesi ambayo iliibwa na hakimu naye alikuwa na ufisadi. Ilikuwa kesi iliyoibwa, fedheha. Hawakuweza kupewa sehemu nyingine ya kubadili. Tulikuwa na 5% au 6% katika wilaya hii, katika eneo hili. Hii iliibwa, kesiya fedheha,” taarifa ya Trump imesema.

Spika wa Baraza la Wawakilishi, Mike Johnson, Mrepublican wa ngazi ya juu amesema katika taarifa, “Leo ni siku ya aibu katika historia ya Marekani. Wademocrat wanashangilia wakati kiongozi anapokutwa na hatia ya upande wa upinzani kwa mashtaka ya kejeli, yaliyotolewa kwa ushahidi wa uongo, mhalifu aliyehukumiwa. Hili lilikuwa suala la kisiasa, na siyo la kisheria.”

Wabunge Wademocrat amesema hatia – iliyojadiliwa na majaji 12 – imethibitisha nguvu ya mfumo wa kisheria wa Marekani.

“Mtu ambaye amekutwa na hatia ya makossa 34 ya uhalifu na hajaonyesha heshima yeyote kwa mfumo wa sheria hafai kuongoza taifa kubwa duniani,” amesema Seneta Mdemocrat Sheldon Whitehouse, mwenyekiti wa kama ndogo ya sheria katika Seneti.

“Ni ukweli pekee katika vyumba vya mahakama kwambarais wa zamani ameshindwa kudanganya na kujitoa katika matatizo yanayomkabili. Wamarekani wanawaamini wanachama wa opo kwa sababu nzuri.”

Hatia imebainisha kuwa ni rais wa kwanza wa zamani wa Marekani kukutwa na hatia ya uhlifu. Uamuzi, hata hivyo, haumzuii Trump kuwania urais, na anakabiliwa na mchakato mrefu wa rufaa.

Barbara Perry, mwenyekiti mwenza wa Presidential Oral History Program katika chuo kikuu cha Virginia, kituo cha Miller, ameiambia VOA kwamba kama rufaa atashindwa katika rufaa, Trump ataweka historia nyingine kwa rais wa Marekani.

Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump baada ya jopo la mahakama kumpata na hatia.
Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump baada ya jopo la mahakama kumpata na hatia.

“Hebu sote tumese kwamba hatia hii ya uhalifu ikisimama hadi Novemba 5, siku ya uchagui ujao wa rais.

Itakuwa nikwamba kama ataendelea kuishi katika makazi yake ya Florida, jimboambalo mtuhumiwa wa uhalifu haruhusiwi kupiga kura, kwa hiyo kimsingi hataruhusiwa kujipigia kura. Jambo jingine zito, kwa kuongezea , nikwamba Warepublican wengi kiasili katika miaka ya karibuni wamejaribu kukandamiza kura.”.

Trump huenda pia akakabiliwana kifungo au huenda akawekwa kwenye kizuizi cha nyumbani kama hatia yake itaendelea kama ilivyo.

Seneta Mrepublican Lindsey Graham amekosoa mchakato ambao ulimkuta na hatia.

Forum

XS
SM
MD
LG