Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 09:53

Nikki Haley asema atampigia kura Donald Trump katika uchaguzi mkuu ujao


Balozi wa zamani wa Umoja wa Mataifa Nikki Haley akizungumza katika Taasisi ya Hudson mjini Washington Dc, Jumatano, Mei 22, 2024. (AP).
Balozi wa zamani wa Umoja wa Mataifa Nikki Haley akizungumza katika Taasisi ya Hudson mjini Washington Dc, Jumatano, Mei 22, 2024. (AP).

Haley alifunga  kampeni yake mwenyewe ya uteuzi wa chama hicho cha Republikan  miezi miwili iliyopita. Haley na Trump walikosoana  vikali wakati wa mchujo wa chama chao.

Nikki Haley anasema atampigia kura Donald Trump katika uchaguzi mkuu ujao akimhimiza mteule mtarajiwa wa chama cha Republikan kufanya bidii ili kupata uungwaji mkono kutoka kwa wale waliomuunga mkono yeye Nikki katika uchaguzi wa awali.

Haley alitoa maoni hayo Jumatano wakati wa hafla katika Taasisi ya Hudson huko Washington. Haley alifunga kampeni yake mwenyewe ya uteuzi wa chama hicho cha Republikan miezi miwili iliyopita lakini hakumuidhinisha Trump mara moja. Wagombea wote wawili walikosoana vikali wakati wa mchujo wa chama chao.

Forum

XS
SM
MD
LG