Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 10:04

Rais Biden amkaribisha kiongozi wa Kenya William Ruto White house

Rais wa Marekani Joe Biden (Kulia) na Rais wa Kenya William Ruto (kushoto) wakishiriki katika hafla pamoja na Wakurugenzi Wakuu na viongozi wa biashara katika Ikulu ya Marekani mjini Washington, DC Mei 22, 2024. (Picha na Mandel NGAN/AFP

Rais wa Marekani Joe Biden alisema anapanga kufanya ziara rasmi barani Afrika mwezi Februari baada ya uchaguzi wa rais wa Marekani, tangazo ambalo linabashiri kuwa atamshinda Donald Trump.

"Ninapanga kwenda mwezi Februari baada ya kuchaguliwa tena," Biden alisema alipokuwa akimsalimia Rais wa Kenya William Ruto alipowasili Ikulu katika siku ya kwanza kati ya mbili za mikutano na chakula cha jioni.

Maafisa wakuu wa utawala walisema Biden na Ruto watajadili masuala mbalimbali kutoka biashara hadi msamaha wa madeni na njia ya kusonga mbele kwa ajili ya Haiti, Ukraine, Sudan na maeneo mengine.

Biden, ambaye ni Mdemokrat, anawania muhula mwingine katika uchaguzi wa Novemba 5 dhidi ya mpinzani wake wa chama cha Republican, Rais wa zamani Donald Trump.

Forum

XS
SM
MD
LG