Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 00:58

Biden kupitisha amri ya kiutendaji kwa ajili ya uhamiaji


Rais wa Marekani Joe Biden.
Rais wa Marekani Joe Biden.

Vyombo vya habari vya Marekani vimesema kuwa rais wa Marekani Joe Biden Jumanne atazindua  amri ya kiutendaji ambayo itapunguza kwa  idadi kubwa  watu wanaoomba hifadhi kwenye mpaka wa Marekani na Mexico.

Kulingana na maafisa wa utawala, amri hiyo itapelekea kufungwa kwa mpaka mara idadi ya wahamiaji inapofikia 2,500. Amri hiyo itaanza kufanya kazi mara moja baada ya kutiwa saini, kwa kuwa idadi ya waomba hifadhi kwa sasa tayari imevuka viwango.

Biden anatoa amri hiyo chini ya sheria ya kitaifa ya uhamiaji iliyopitishwa miaka 72 iliyopita, maarufu kama 212(f), ambayo inatoa mamlaka kwa rais kuzuia kuingia nchini kwa wahamiaji wa kila tabaka, wanaoaminika kuhatarisha maslahi ya Marekani.

Rais wa zamani Donald Trump alitumia sheria hiyo kuchukua baadhi ya hatua kali dhidi ya wahamiaji ikiwemo ile ya iliozuia wahamiaji kutoka mataifa 7 ya kiislamu. Trump ameahidi kutumia sera kali za uhamiaji, iwapo atachaguliwa tena kwenye uchaguzi wa Novemba.

Forum

XS
SM
MD
LG