Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 22:16

Mahakama ya rufaa ya Georgia yasitisha kwa muda kesi ya jinai dhidi ya Trump


Rais wa zamani wa Marekani Donald akizungumza katika kampeni katika ukumbi wa Forum River Center, Georgia, Machi 9, 2024. Picha ya Reuters
Rais wa zamani wa Marekani Donald akizungumza katika kampeni katika ukumbi wa Forum River Center, Georgia, Machi 9, 2024. Picha ya Reuters

Mahakama ya rufaa katika jimbo la Georgia Jumatano ilisitisha kwa muda, kesi ya jinai inayomtuhumu Donald Trump kutaka kubatilisha matokeo ya uchaguzi wa 2020, huku ikizingatia ombi la rais huyo wa zamani la kumuondoa mwendesha mkuu Fani Willis katika usimamizi wa kesi hiyo.

Amri hiyo inazuia kesi inayoendelea dhidi ya Trump na washtakiwa wenza 14 kufikishwa mahakamani, huku Trump akikata rufaa dhidi ya uamuzi wa Jaji, unaomruhusu Willis, wakili wa wilaya ya Kaunti ya Fulton, kuendelea kusimamia kesi.

Ni ishara nyingine kwamba kesi hiyo, moja kati ya nne zinazomkabili Trump anayetaka kumvua madaraka Rais Joe Biden na kurudi White House, haitasikilizwa kabla ya uchaguzi wa tarehe 5 Novemba.

Jopo la Mahakama ya New York wiki iliyopita lilimpata Trump na hatia ya kuficha malipo ya kumnyamazisha mwanamke mcheza filamu za ngono, uamuzi ambao Trump ameapa atakata rufaa kuupinga.

Forum

XS
SM
MD
LG