Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 08:32

Trump arejea katika kampeni akiwa rais wa kwanza kupatikana na hatia ya uhalifu


Mgombea urais wa Republikan, Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump akiwa katika kampeni ya uchaguzi huko Las Vegas, Nevada, Juni 9, 2024.
Mgombea urais wa Republikan, Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump akiwa katika kampeni ya uchaguzi huko Las Vegas, Nevada, Juni 9, 2024.

Donald Trump amerejea kwenye kampeni ya kisiasa wiki hii akiwa rais wa kwanza wa Marekani kukutwa na hatia ya uhalifu wakati ambapo ni mgombea mkuu wa chama.

Mwandishi wa VOA Scott Stearns anaangalia jinsi wapiga kura wanavyojibu hatia yake kwenye mikutano ya kampeni.

Wafuasi wa Donald Trump waliendelea kumshangilia mgombea wao nje ya jengo ya Trump Tower huko New York siku moja baada ya rais wa zamani kukutwa na hatia kwa makossa 34 ya uhalifu kwa kugushi rekodi za biashara katika nja ma ya kufanya ushawishi kinyume cha sheria kwa ajili ya matokeo ya uchaguzi wa mwaka 2016.

Katika ujirani wa Chelsea, mpiga kura Nicholas Warner anasema kukutwa na hatia “ni jambo baya sana” nchi inamhitaji Trump wa awamu ya pili.

Nicholas Warner, Mpiga Kura mkaazi wa New York anasema: “Alipokuwa madarakani kwa miaka minne, tulikuwa hatuna kile ambacho tunakipitia hivi sasa, vita, na kila kitu kingine, na usisahau, unajua, uchumi na mfumuko wa bei. Kwahiyo ningependa arejee tena, na kushughulikia masuala ya kibiashara kama mfanyabiashara.”

Huko Maryland, mpiga kura Arkady Lapidus anasema madai ya Trump kwamba kesi yake iliibwa si mazuri kwa chama cha Republican au kwa nchi.

Arkady Lapidus, Mpiga Kura, mkaazi wa Maryland anaeleza: “Hakuna kitakachotokea mpaka kiachane na Donald Trump, tunaamini katika uchaguzi. Tunaziamini mahakama, tunawaamini wanachama wa jopo la kisheria ambao walitoa maamuzi kwasababu ni wamarekani wenzetu. Mpaka chama kwa ujumla kikumbatie thamini za Marekani kama ninavyoziona, kamwe sitakipigia kura chama cha Republican.”

Mpiga kura Margaret Barnes anasema kwamba hata kwa kukutwa na hatia ya uhalifu, Trump anaaminiwa zaidi kuliko Joe Biden.

Margaret Barnes, Mpiga Kura na mkaazi Maryland: “Biden, kwa kweli mimi ninavyomuona ni fake na pia ni fake kihisia, kuelezea hadhithi kama vile mtu mzima mzuri, unajua, si uhalisia. Simuamini. Si mkweli. Na Trump, ana vishindo. Lakini ingawaje kile anachokisema kinakuwa na uchokozi, namuamini sana.”

Huko Colorado, mpiga kura Luda Golodnykh anasema hatia ya Trump inamstahili, ana matumaini itaumiza kampeni yake.

Luda Golodnykh, Mpiga Kura, Colorado anaeleza: “Jinsi anavyozungumza huku wanawake, jinsi anavyozitendea nchi nyingine, jinsi anavyozungumza kuhusu wahamiaji haramu, yeye kuoa mhamiaji, pia. Nasema, ndiyo, nadhani.”

Huko Nevada, mpiga kura Keith Dayton anasema hatia haina matokeo kwa kura yake.

Keith Dayton, Mpiga Kura, Nevada anasema: “Bado nitampigia kura Donald Trump. Nadhani jambo lote lilikuwa ni kituko tu. Nimetiwa aibu na nchi yetu.”

Keith Dayton, Mpiga Kura, Nevada anasema: “Mimi hata sitamkaribisha kuja kunywa bia au kwenda klabu nay eye.”

Katika jimbo ambalo linaweza kuelemea upande wowote la Pennyslvania, hatia aliyokutwa nayo Trump huenda ikawatia hamasa wafuasi wake anase,a Jeffrey Nesbitt.

Jeffrey Nesbitt, Mpiga Kura, Pennsylvania: “Nadhani itakuwa na ufanisi zaidi kwa watu wa Marekani kumpiga na harakati zake katika boksi la kura. Nadhani kuna uwezekano mzuri kuwa hatia hii huenda ikatia moyo harakati zake na kujitokeza na kupiga kura kwa ujasiri zaidi na kitendo cha uchukozi katika chaguzi zijao.”

Asilimia 90 ya wa Republican waliojiandikisha bado wanamuunga mkono Trump, kwa mujibu wa ukusanyaji maoni ulioanywa na Reuters na Ipsos. Asilimia kumi iliyobaki ya Warepublican hivi sasa si rahisi kumpigia kura Trump na huenda hilo linaweza kuleta tofauti katika uchaguzi wa karibu ambapo wagombea wote wawili wanahitaji kushikilia ngome zaidi na kuwapata wapiga kura huru.

Forum

XS
SM
MD
LG