Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 18:46

Michael Cohen anatarajiwa kutoa ushahidi Jumatatu dhidi ya Donald Trump


Michael Cohen, wakili wa zamani wa Donald Trump.
Michael Cohen, wakili wa zamani wa Donald Trump.

Cohen alifanya kazi na Trump huko New York kabla ya Trump kuwa mwanasiasa.

Michael Cohen, ambaye alikutwa na hatia ya kudanganya, na pia wakili wa zamani na muwekaji sawa masuala ya kisiasa wa wakati mmoja kwa Donald Trump, anatarajiwa kutoa ushahidi Jumatatu dhidi ya aliyekuwa rais wa Marekani.

Cohen mwenye miaka 57 alifanya kazi na Trump, mfanyabiashara wa uuzaji nyumba huko New York nchini Marekani tangu mapema miaka ya 2000 kabla ya Trump kuwa mwanasiasa. Cohen aliwahi kujiita “mhuni aliyeandaliwa” wa Trump na alitabiriwa katika ushahidi wa bunge kwamba kwa miaka mingi alikuwa ametoa vitisho 500 kwa watu kwa amri ya Trump.

Trump ambaye hivi karibuni mwaka 2017, ulikuwa mwaka wake wa kwanza wa urais, alimuelezea Cohen kama “mwanasheria mahiri” na “mwanasheria mzuri katika kampuni yake”.

Forum

XS
SM
MD
LG