Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Novemba 22, 2024 Local time: 18:10

Rais wa zamani Trump huenda akakabiliwa na kifungo jela baada ya kukutwa na hatia ya kugushi


Rais wa zamani na mgombea urais wa Chama cha Republikan Donald Trump akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukutwa na hatia katika kesi ya uhalifu katika Mahakama ya Manhattan, New York City, on Mei 30, 2024.
Rais wa zamani na mgombea urais wa Chama cha Republikan Donald Trump akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukutwa na hatia katika kesi ya uhalifu katika Mahakama ya Manhattan, New York City, on Mei 30, 2024.

Mchakato wa kisheria unaonyesha hali ya kutokuwa na uhakika kwa kampeni yake na nafasi yaka katika uchaguzi ujao.

Donald Trump alikutwa na hatia ya kugushi rekodi za biashara kama sehemu ya njama ya kukandamiza habari mbaya kabla ya kuchaguliwa kwake mwaka 2016.

Amekutwa na hatia wakati wa kampeni hii ya urais, maamuzi yazua maswali jinsi Trump atakavyoendelea na kampeni kama atapelekwa gerezani. Mwendesha mashtaka wa zamani Steven Cohen hatarajii kuwa Trump atafungwa jela karibuni.

Steven M. Cohen, Profesa wa Sheria New York: “Kutakuwa na hoja nzito baada ya kesi na halafu kutakuwa na rufaa na rufaa hiyo itachukua miezi kadhaa, kama siyo zaidi ya mwaka. Kwahiyo, nadhani mengi yatajitokeza katika harakati za kisiasa kuliko habari zitakazotoka, walau awali, kuhusu hatima ya Donald Trump na matokeo ya hatia yake.”

Trump atahukumiwa Julai 11, watalaamu wa sheria wanasema muda wowote atakaohukumiwa kuwa gerezani huenda ukawa chini sana kuliko kifungo cha juu cha miaka 20.

Joseph Tully, Wakili wa Utetezi: “Kutokana na miaka yake, hasa ikizingatiwa hana rekodi ya uhalifu na hapa matokeo yanajieleza yenyewe kwa kweli hatazamii adhabu ya muda mrefu au adhabu kali.”

Wengine wanazungumzia kifungo ambacho mwanasheria wa zamani wa Trump Michael Cohen ambacho amekaa gerezani, ni kielelezo cha hukumu ya Trump.

Abbe Smith, Mwanasheria wa Georgetown: “Ni nadra sana kwa mtu wa chini katika njama kupewa kifungo cha jela na mkuu wake hapewi. Donald Trump alikuwa juu katika njama ya uhalifu. Kwahiyo, jaji anaweza kumhukumu kifungo Bwana Trump.”

Njia mbadala kwa kifungo ni kuwa katika uangalizi, kifungo cha nyumbani na faini. Lakini huenda kifungo chochote kile hakitatekelezwa mpaka baada ya mchakato wa rufaa, ambao huenda ukafanyika baada ya uchaguzi wa Novemba.

Adhabu yoyote ile itakayotolewa mwezi ujao, itatoa habari kwa kesi tatu za uhalifu ambazo bado hazijamalizika dhidi ya Trump.

Preet Bharara, Mwanasheria wa Zamani wa Southern District of New York: “Ukweli kuhusu hatia hii, ni kama bado iko katika vitabu, huenda ikapelekea adhabu ya kifungo kikubwa jela katika kesi zijazo. Kwahiyo ina matokeo yake, kwasababu itakuwa sasa, kinyume na ilivyokuwa wiki moja iliyopita, ana rekodi ya uhalifu. Rekodi ya uhalifu inazingatiwa katika kutolewa kwa adhabu.”

Mashtaka mengine katika serikali kuu na majimbo yanamkabili Trump, kesi ya Florida kwa wale waliohusika kwa jinsi walivyoshughulikia vibaya nyaraka za siri nayo imecheleweshwa zaidi.

Forum

XS
SM
MD
LG