Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 11:02

Biden akamilisha ziara ya Ufaransa kwa kutembelea makaburi ya wanajeshi wa Marekani


Rais wa Marekeni Joe Biden akitembele makaburi ya Aisne-Marne yaliopo Belleau, Kaskazini mwa Ufaransa. Juni 9, 2024.
Rais wa Marekeni Joe Biden akitembele makaburi ya Aisne-Marne yaliopo Belleau, Kaskazini mwa Ufaransa. Juni 9, 2024.

Rais wa Marekani Joe Biden leo amekamilisha ziara yake ya Ufaransa kwa kutoa heshima zake  kwenye makaburi ya wanajeshi wa Marekani, hatua ambayo rais wa zamani Donald Trump aliepuka wakati alipokuwa madarakani.

Biden amechukua hatua hiyo akiwa na matumaini kwamba huenda ikamsaidia kwenye uchaguzi mkuu wa Novemba. Biden alitembelea makaburi hayo ya Aisne-Marne ambayo yako nje ya mji wa Paris. Aliweka shada la maua kwenye kanisa lililopo hapo ambako zaidi ya wanajeshi 2,200 wa Marekani waliokufa kwenye vita vya kwanza vya Dunia wamezikwa.

Ziara ya Biden pia imefanyika wakati wa maadhimisho ya 80 ya siku ya D-Day ambayo husherehekea ushirikiano kati ya Marekani na Ufaransa. Wakati wa ziara ya Trump ya 2018 nchini Ufaransa, aliepuka kutembelea makaburi hayo ,huku White House ikisema kuwa ilikuwa ni kutokana na hali mbaya ya hewa.

Hata hivyo ripoti zilizotolewa baadaye zilisema kuwa Trump alisusia kuiyatembelea kutokana na kuwa aliona wanajeshi waliozikwa huko kama watu walioshindwa. Trump amekuwa akikanusha ripoti hizo ingawa zilithibitishwa na msemaji wa Ikulu wa wakati huo John Kelly.

Forum

XS
SM
MD
LG