Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Juni 26, 2024 Local time: 21:02

Rais Biden akutana na Rais Zelenskyy


Rais wa Marekani, Joe Biden, amekutana na Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy, jijini Paris, leo Ijumaa na kutangaza  msaada mpya wa silaha wenye thamani ya  dola milioni 225.

Mkutano huo umefanyikam pembezoni mwa sherehe za kumbukumbu ya D Day.

Hayo yalikua mazungumzo yao ya kwanza ya ana kwa ana toka Zelenskyy, alipotembelea Washington, mwezi Desemba, wakati wawili hao walipokabiliana na upinzani wa chama cha Republican, katika kutoa msaada zaidi kwa Ukraine.

Watakutana tena wiki ijayo katika mkutano wa G7, nchini Italia, huku mataifa tajiri yakijadili kutumia Mali za Russia, zilizo shikiliwa baada ya uvamizi wa Ukraine, kupata dola bilioni 50 kusaidia Ukraine.

Zelenskyy, aliiambia Reuters mwezi uliopita kwamba nchi za Magharibi zinachukua muda mrefu kufanya maamuzi kuhusu misaada.

Forum

XS
SM
MD
LG